NA YEREMIAS NGERANGERA -NAMTUMBO
Wanachama
wa chama cha mapinduzi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wamemchagua
Aggrey Mwansasu kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kwa kumbwaga
aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Benjamini Nindi .
Uchaguzi
wa kumpata mwenyekiti huyo ulifanyika katika Bwalo la shule ya
sekondari Namtumbo shule ambayo inamilikiwa na jumuiya ya wazazi wa
chama cha mapinduzi kilomita tatu kutoka mjini Namtumbo.
Aidha
katika uchaguzi huo awali uliingia dosari baada ya msimamamizi wa
uchaguzi huo Zena Rashidi Mijinga kujisahau kwa kutosoma kanuni ya
kushinda uchaguzi ni sharti mgombea apate asiliomia hamsini ya kura
zitakazopigwa.
Dosari
ya kanuni hiyo kutosomwa awali ilijionesha baada ya wagombea wa nafasi
ya uenyekiti kutofikia asilimia hamsini ya kura zilizopigwa na kuwataka
wajumbe wa mkutano huo kurudia kupiga kura kwa nafasi ya uenyekiti hali
iliyoibua hasira kutoka kwa wajumbe kwa madai ya kutaka kumbeba mgombea
mmojawapo katika uchaguzi huo na kuongeza kuwa kanuni hizo kwa nini
hazikusomwa kabla ya uchaguzi na badala yake zisomwe wakati uchaguzi
umefanyika.
Mwenyekiti
wa muda wa mkutano huo bwana Fadhili Kitete alionekana kuokoa jahazi
kutoka kwa wajumbe waliotaka kukataa kurudia uchaguzi huo kwa kuwaomba
wajumbe hao radhi kwa kutosoma kanuni hizo kabla ya uchaguzi na kusema
kuwa ni kosa la kibinadamu na kuwataka wajumbe waridhie kurudia kupiga
kura kwa nafasi hiyo ya uenyekiti kwa kuzingatia kanuni hiyo ya asilimia
Hasini ili uchaguzi huo uwe wa haki na uliofuata kanuni za uchaguzi.
Bwana
kitete aliongeza kuwa kanuni ndizo zinazoongoza uchaguzi na kurudia
uchaguzi hautazuia wajumbe kumchagua mgombea wanayempenda alisema
mwenyekiti huyo wa muda wa uchaguzi huo.
Wajumbe
kwa pamoja walikubaliana na hoja ya Mwenyekiti huyo wa muda kurudia
kupiga kura katika nafasi hiyo ya mwenyekiti wa chama wa wilaya.
Waliogombea
nafasi ya uenyekiti wa chama wilaya ya Namtumbo walikuwa wanne ambao ni
Legani Luambano ,Yordani Fusi,Benjamini Nindi na Aggrey Mwansasu ambapo
katika uchaguzi wa awali Legani Luambano alipata kura 20, Yordani Fusi
alipata kura 25, Benjamini Nindi aliyekuwa akitetea kiti hicho alipata
ura 290 na Aggrey Mwansasu alipata kura 304 kati ya kura 645
zilizopigwa.
Uchaguzi
wa marudio uliwashindanisha wagombea wawili Benjamini Nindi na Aggrey
Mwansasu ambao walionesha kuwa na ushindani mkubwa kwa wajumbe lakini
mpaka mwisho wa uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi huo Zena Rashidi
alimtangaza Aggrey Mwansasu kuwa mshindi kwa nafasi ya uenyekiti kwa
kumbwaga mpinzani wake Benjamini Nindi aliyekuwa anatetea nafasi hiyo
kwa awamu nyingine tena.
Zena
Rashidi alimtangaza Aggrey Mwansansu ameshinda nafasi hiyo kwa kupata
kura 369 dhidi ya kura 228 alizopata mpinzani wake kati ya kura 610
zilizopigwa ambapo kura 13 ziliharibika katika uchaguzi huo .Mkutano
huo pia uliwachagua wajumbe wawakilishi wa mkutano mkuu wa
Taifa,mkutano mkuu wa mkoa na viongozi wa jumuiya ya wanawake, vijana na
wazazi.


Post a Comment