Meneja Mauzo wa Jumia Tanzania, Iddy Mkumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Black
Friday utakaoweza kutoa punguzo la asilimia 70 kwa bidhaa atakayoinunua
mteje kupitia tovuti ya Jumia Tanzania itakayoanza mwezi
wa Novemba 24 hadi Desemba 04 mwaka huu kwa mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mwanza,Morogoro, Mara na
Zanzibar.
Afisa
Masoko na Mahusiano ya Jamii wa Jumia Travel, Geofrey Kijanga,
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Jumia Travel inavyotoa huduma
za malazi na namna walivyopunguza bei kwa msimu huu wa sikukuu leo
kwenye ofisi za Jumia Tanzania jijini Dar Es Salaam
Maneja
Masoko wa Jumia Tanzania, Albany James(kulia) akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu jinsi Kampuni ya Jumia Tanzania akizungumzia kuhusu
siku ya Black Friday itakayofanyika kwa takribani siku kumi na moja (11)
kuanzia mwezi wa Novemba 24 hadi Desemba 04 mwaka huu.
Mkutano ukiendelea kwenye ukumbi wa ofisi ya Jumia Tanzania jijini Dar es Salaam leo
Ikiwa
imebaki takribani miezi miwili mwaka 2017 kuisha, Jumia Tanzania
imejizatiti kuja na kampeni iliyopewa jina la ‘BLACK FRIDAY’ ambayo
itawawezesha wateja wake kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali mtandaoni
kwa punguzo la mpaka alisimia 70 kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 4
mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu ujio wa kampeni hiyo Meneja Mauzo wa
Jumia Tanzania, Bw. Idd Mkumba amebainisha kuwa kutokana na mafanikio
makubwa ya kampeni hiyo iliyofanyika mwaka jana na kushuhudia watanzania
wakifanya huduma za mtandaoni ambapo takribani oda 600 kwa siku wameona
ni vema kuirejesha tena kwa kishindo mwaka huu.
“Mwaka
2016 ulikuwa ni wenye mafanikio kwa upande wa kampeni yetu ya BLACK
FRIDAY kwani ndani ya muda wa siku tano tuliyoifanya wateja wengi
waliweza kufanya manunuzi mtandaoni. Hivyo basi kwa mwaka huu tena
tumeiboresha Zaidi kwa kuongeza siku kutoka tano mpaka 11 ambapo kampeni
itaanza rasmi kuanzia Novemba 24 mpaka Desemba 4.
Na kwa kuongezea hapo ni kwamba safari hii wateja wa Dar es Salaam hawatofaidika pekee yao kwani tumejitanua Zaidi mpaka mikoa mingine kwa mara ya kwanza na kuzifikia sehemu za Visiwani Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Iringa na Musoma,” alisema Bw. Mkumba.
Na kwa kuongezea hapo ni kwamba safari hii wateja wa Dar es Salaam hawatofaidika pekee yao kwani tumejitanua Zaidi mpaka mikoa mingine kwa mara ya kwanza na kuzifikia sehemu za Visiwani Zanzibar, Dodoma, Mwanza, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Iringa na Musoma,” alisema Bw. Mkumba.
Meneja
Mauzo huyo wa Jumia Tanzania aliendelea kwa kufafanua kuwa, “Lengo
kubwa la kampeni hii ni kuhakikisha kwamba tunawajengea uwezo na
kuwarahisishia watanzania kufanya huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao
mahali popote walipo huku wakiendelea na shughuli zao.
Tanzania ni mojawapo ya taifa linaloendelea Afrika na duniani likiwa na watumiaji wa simu za kisasa na mtandao wa intaneti wanaoongezeka kila kukicha. Hivyo basi nasi tunaitumia fursa hiyo kwa kuwahamisisha watanzania kuitumia teknolojia hiyo kwa manufaa Zaidi, ambapo badala ya kutumia muda mwingi kwenda madukani wanaweza kufanya hivyo wakiwa palepale walipo.”
Tanzania ni mojawapo ya taifa linaloendelea Afrika na duniani likiwa na watumiaji wa simu za kisasa na mtandao wa intaneti wanaoongezeka kila kukicha. Hivyo basi nasi tunaitumia fursa hiyo kwa kuwahamisisha watanzania kuitumia teknolojia hiyo kwa manufaa Zaidi, ambapo badala ya kutumia muda mwingi kwenda madukani wanaweza kufanya hivyo wakiwa palepale walipo.”
“Katika
kuwaondoa hofu wateja ambao wanahofia kwamba pengine bidhaa zinaweza
kuwa hazina ubora kutokana na ukubwa wa ofa tunazotoa, ni kwamba Jumia
Tanzania tunafanya huduma zetu kwa sera ya kulipia pale unapopokea
bidhaa yako. Hii humpatia mteja kujiridhisha kwamba bidhaa aliyoiagiza
ni sahihi ndipo alipie. Na kwa kuongezea, ada ya malipo ya kufikishiwa
mzigo kwa wateja wetu popote walipo itashuka ili kuhamasisha manunuzi
Zaidi.
Kwa kumalizia kuhusiana na kampeni ya BLACK FRIDAY ambayo itawapatia fursa wateja kupata punguzo la bei mpaka la asilimia 70, tumeingia ubia na makampuni kadhaa makubwa ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa kama vile Samsung, Startimes, Tronic,… Lakini pia kutokana na kuanza kwa huduma kwenye mikoa mipya niliyoiorodhesga hapo juu, tumetoa ofa kwa wateja watakaofanya manunuzi ya kuzidi shilingi 100,000 watajipatia punguzo la 50% ambapo itawabidi watumie neonsiri J695D,” alihitimisha Bw. Mkumba.
Kwa kumalizia kuhusiana na kampeni ya BLACK FRIDAY ambayo itawapatia fursa wateja kupata punguzo la bei mpaka la asilimia 70, tumeingia ubia na makampuni kadhaa makubwa ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa kama vile Samsung, Startimes, Tronic,… Lakini pia kutokana na kuanza kwa huduma kwenye mikoa mipya niliyoiorodhesga hapo juu, tumetoa ofa kwa wateja watakaofanya manunuzi ya kuzidi shilingi 100,000 watajipatia punguzo la 50% ambapo itawabidi watumie neonsiri J695D,” alihitimisha Bw. Mkumba.
Akifafanua
Zaidi juu ya dhana nzima ya kampeni hiyo, Meneja Masoko wa Jumia
Tanzania, Bw. Albany James amesema kuwa utamaduni wa BLACK FRIDAY
umeanzia nchini Marekani ambapo makampuni wafanyabiashara hutoa punguzo
la bei za bidhaa na huduma mbalimbali ili kuukaribisha msimu wa
mapumziko na Krisimasi.
“Utamaduni
huu wa kufanya punguzo kubwa la bei mbalimbali za bidhaa na huduma
ulianzia nchini Marekani na kushika kasi sehemu zingine duniani kutokana
na faida kubwa kwa wafanyabiashara na wateja kwa ujumla. Ni kipindi
ambacho watu wengi hufanya maandilizi ya msimu wa sikukuu za Krisimasi
na Mwaka Mpya. Na nadhani utamaduni huo hata kwa sisi watanzania pia
tunautumia hivyo basi kupitia Jumia Tanzania wateja wataweza kununua
bidhaa mbalimbali muhimu kwa msimu huo kama vile za nyumbani, umeme,
mavazi, vyombo vya kupikia nakadhalika. Kwa hiyo ningependa kuwatoa hofu
wateja wetu kwamba ni bei za bidhaa ndizo zitakazopungua na sio ubora
kama wengi wanavyodhahania,” alisema na kumalizia Bw. James.
Katika
kunogesha kampeni hii Jumia Tanzania pia imeshirikiana na makampuni
tanzu ya Jumia hapa nchini kama vile Jumia Travel na Jumia Food ambayo
nayo yanajihusisha na huduma kwa njia ya mtandao. Ushirikiano huo
utawapatia faida wateja watakaokuwa wakifanya manunuzi mtandaoni kupata
ofa kama vile za malazi ya bure pamoja na punguzo kubwa kwa hoteli
mbalimbali za kifahari nchini.
Akizungumza
kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Umma na Masoko wa Jumia Travel
Tanzania, Bw. Geofrey Kijanga ameelezea kuwa wao kama watoaji wa huduma
za hoteli kwa njia ya mtandao mbali na kutoa ofa ya kulala bure kwenye
hoteli kwa wateja lakini pia watatoa punguzo kubwa la bei za huduma za
malazi ambalo litadumu mpaka mwezi Desemba.
“Tunafahamu
kwamba tunaelekea kuumaliza mwaka ambao hugubikwa na msimu wa mapumziko
na sikukuu za Krisimasi na Mwisho wa Mwaka, suala la watu kwenda
kutembelea na kupumzika sehemu mbalimbali ni muhimu. Katika
kulirahisisha hilo Jumia Travel itatoa punguzo kubwa la huduma za malazi
kwa hoteli inazofanya nazo kazi nchini. Kwa hiyo mteja hatowaza kuhusu
gharama za malazi popote atakaposafiri yeye au pamoja na familia yake.
Hivyo basi ni muda muafaka kwa watanzania kuzitumia ofa hizi kwani huwa
ni za kweli na hurahisisha gharama kubwa ambazo wanaweza kuziingia
kuzipata kwa njia nyinginezo za kawaida,” alisema na kuhitimisha Bw.
Kijanga.
Hii ni
fursa kwa watanzania wote kwa ujumla kujiaandaa vema na msimu wa
mapumziko na sikukuu unaokuja kwa kufanya manunuzi ya gharama nafuu
Zaidi mahali popote walipo kuanzia Novemba 24 na kuendelea kwa siku 11
mwaka huu. Ili kufahamu Zaidi na kujua mengi juu ya ofa zitakazotolewa
watanzania wanatakiwa kuwa kutembelea mitandao ya Jumia Tanzania pamoja
na kurasa zao za mitandao ya kijamii. Lakini pia kutakuwepo na zawadi
mbalimbali kupitia njia za vocha na kuponi kwa wale watakaokuwa
wakifuatilia kurasa hizo kwa karibu na kujibu maswali mbalimbali.

Post a Comment