Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa
Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa tatu kushoto), wakati alipokagua daraja la
Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya
Sumbawanga, mkoani Rukwa
Meneja
wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina
(wa tatu kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliyevaa fulana nyeusi), wakati
alipokagua daraja la Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM
31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Mafundi
wakiendelea na kazi ya ujenzi wa daraja la Kinambo lililopo katika
barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Muonekano wa mitambo ya kuchimbia nguzo za Daraja la Mto Momba unaounganisha mikoa ya Rukwa na Songwe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Groups)
Corporation, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Momba
linalounganisha mikoa ya Rukwa na Songwe
Mbunge
wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha, akifafanua jambo kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati wa
mkutano na wananchi wa Kilymatundu mara baada ya kukagua ujenzi wa
Daraja la Mto Momba, wilayani Sumbawanga.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza
na wananchi wa Kilymatundu mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
Daraja la Mto Momba, wilayani Sumbawanga.
Mmoja
wa wananchi wa kijiji cha Kilyamatundu kilichopo wilayani Sumbawanga
akimkabidhi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa, ushahidi wa picha za miti iliyokatwa katika shamba lake kupisha
mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto Momba, mkoani Rukwa.
……………….
Imeelezwa
kuwa kukamilika kwa Daraja la Mto Momba linalounganisha mikoa ya Rukwa
na Songwe kutafufua fursa za kiuchumi katika mikoa ya magharibi na
kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema hayo
leo alipokagua ujenzi wa daraja hilo na kuwahakikishia wananchi wa
Wilaya ya Sumbawanga kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha daraja hilo
linakamilika mwezi Agosti mwakani.
“Toeni
ushirikiano unaostahili kwa mkandarasi ili Daraja hili la Momba na
madaraja madogo saba yanayojengwa katika barabara ya
Kasansa-Kilyamatundu yenye urefu wa KM 210.38 yakamilike kwa wakati”,
amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amesisitiza nia ya Serikali ya kujenga barabara ya
Kasansa-Kilyamatundu KM 210.38 na Stalike-Kilyamatundu-Mloo KM 500 kwa
kiwango cha lami ili kuongeza kasi ya uzalishaji na usambazaji wa mazao
ya kilimo na mifugo katika Bonde la Mto Rukwa kwenda maeneo mingine ya
nchi.
“Wale
wote ambao wamewekewa alama za kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa
barabara nawaomba wafanye hivyo mapema ili kuwawezesha wakandarasi
kufanya kazi zao kwa uhuru na kuiwezesha TANROADS kufanya usanifu wa
kina”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye
Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng.
Masuka Mkina, amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa watamsimamia kikamilifu
mkandarasi anayejenga Daraja la Momba na madaraja madogo saba katika
barabara ya Kasansa-Kilyamatundu KM 210.38 ili kazi ujenzi huo ukamilike
kwa wakati.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha, amewataka
wananchi watakaopata fursa za ujenzi wa madaraja hayo kuepuka vitendo
vya wizi na hujuma kwa wakandarasi.
Amesema
kukamilika kwa Daraja la Momba kuna manufaa mengi kiuchumi, kijamii kwa
kuwa daraja hilo litawaunganisha wakazi wa jimbo lake na mkoa wa Songwe
na hivyo kuharakisha shughuli za kimaendeleo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment