Pages

September 24, 2017

YANGA YAITUNGUA NDANDA FC BAO 1-0


BAADA  ya kupata pointi 4 ugenini Yanga yarudi kwa kasi na kufanikiwa kunyakuwa pointi tatu ikiwa nyumbani kwa kuifunga Ndanda ya Mtwara goli 1-0.

Yanga wakiwa nyumbani waliweza kumiliki mpira kwa dakika zote 45 za kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Ibrahim Ajib dakika ya 35.

Kutokana na matokeo ya leo Yanga wanakuwa sawa na Simba kwa pointi wakitofautiana kwa magoli ya kufunga.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Yanga, Shedrack Nsajigwa amesema watafanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza licha ya kupata pointi 3.

Nae kocha msaidizi wa Ndanda Musa Mbaya amesema kushindwa kwao leo ni kutokana na ugeni wa wachezaji ambao wameingia kwenye kikosi chao na kupelekea kutoweka muunganiko mzuri hivyo makosa hayo  watayafanyia kazi mapungufu hususani kwenye upande wa ushambuliaji.
 Mshambuliani wa Timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu, akiachia shuti kali kueleka langoni mwa timu ya Ndanda "Wanakuchele", katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa jioni ya leo kwenye dimba la Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 1-0.
 Mabeki wa timu ya Ndanda, wakimdhibiti vilivyo, mshambuliani wa timu ya Yanga, Obrey Chirwa katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa jioni ya leo kwenye dimba la Uhuru, Jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda bao 1-0.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...