Pages

September 24, 2017

JOSHUA NASARI ASEMA YUKO TAYARI KUWEKA REHANI UBUNGE WAKE ILI KUTOA USHAHIDI KWA MADIWANI WALIOHAMA CHADEMA KWENDA CCM

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mh Joshua Nasari amesema yuko tayari kupeleka ushahidi mbele ya Raisi Dkt John Magufuli unaohusu baadhi ya madiwani waliojiuzulu Chadema na kujiunga na CCM kwamba walipewa rushwa kushawishiwa kuachia nafasi zao.

Akizungumza leo katika mkutano na wandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi za chama hicho wilaya ya Arusha mjini,Nasari amesema wakati wowote kuanzia sasa yupo tayari kuweka ubunge wake rehani endapo ushahidi atakaoutoa mbele ya raisi utathibitika kuwa uongo kuhusu madiwani hao.

Amesema ushahidi kwamba baadhi ya madiwani hao wamepewa rushwa umekusanywa na kifaa maalum cha kielectonik Kutoka nchini uingereza alipokuwa masomoni.
Akizungumzia kuhusu suala la uchomaji wa shule katika baadhi ya maeneo ya Arusha yaliyotokea mwaka jana Nasari amesema kuwa uchunguzi alioufanya kupitia amegundua miongoni mwao wapo baadhi ya wateule wa raisi ambao wanatuhumiana kwamba wanahusika.
Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amemuomba raisi akubali ushahidi huo na uwekwe hadharani kama ilivyofanyika kwa ripoti ya Ugunduzi wa wizi wa makinikia .

Haya yanajiri wakati jana baadhi ya madiwani wa chadema kukihama chama hicho na kuhamia chama cha maoinduzi ccm wakidai kumuunga raisi katika utendaji wake kwenye mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...