SHIDA YA MAJI LONGIDO KUWA HISTORIA-MAJ
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye
eneo la uwekaji jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Longido mkoani
Arusha, Septemba 21, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akipokea kirungu ikiwa ni zawadi ya asili ya
Kabila la Wamasai kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Mila wa Tarafa ya
Longido, Thomas Olengulupa kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa
Maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea usinga ikiwa ni zawadi ya asili ya
Kabila la Wamasai kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Mila wa Tarafa ya
Longido, Thomas Olengulupa kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa
Maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa
wa Arusha , Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Longido kabla ya
kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Longido Mkoani Arusha Septemba
21, 2017.
Baadhi
ya Wananchi wa Longido wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa wakati
alipozungumza kabla ya kuweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa
Longido Mkoani Arusha, Septemba 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la Mradi wa maji wa
Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto ni Waziri wa
Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt. Mary Nagu. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuweka jiwe la msingi la
Mradi wa maji wa Longido mkoani Arusha Septemba 21, 2017. Wapili kushoto
ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge na kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Kulia ni Mbunge wa Hanang Dkt.
Mary Nagu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
CHANGAMOTO
ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama wilayani Longido mkoani
Arusha kuwa historia baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuweka jiwe
la msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni
15.8.
Waziri
Mkuu ameweka jiwe hilo la msingi leo (Alhamisi, Septemba 21, 2017) kwa
ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Longido Mjini pamoja na kijiji cha
Oltepesi ambao chanzo chake ni kutoka mto Simba wilaya ya Hai mkoani
Kilimanajro.
Amesema
Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama
ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya
maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye
makazi yao.
Pia
Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson
Lwenge kupeleta wataalamu wilayani Longido ambao watashirikiana na
Halmashuri za wilaya ya Longido na tarafa ya Loliondo kutafuta vyanzo
vingine vya maji ili wananchi waweze kupata maji ya kutosha.
Waziri
Mkuu amesema asilimia kubwa ya wananchi wa wilaya za Longido na
Ngorongoro ni wafungaji hivyo wanahitaji maji mengi watakayoyatumia
katika matumizi yao ya kawaida ya nyumbani pamoja na kunyweshea migugo.
Pia
Waziri Mkuu amewaagiza wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huo pamoja
na miradi mingine midogo tisa katika wilaya ya Longido kutumia vifaa
vinavyotengenezwa na viwanda vya ndani ili kuunga mkono jitihada za
Serikali ya Awamu ya Tano kukuza uchumi kupitia viwanda.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa wazingatie
sheria ya Mazingira inayozuia kufanya shughuli za kibinadamu pamoja na
kujenga kwenye maeneo yote ya vyanzo vya maji ndani ya mita 60 ili
kuliepusha Taifa kugeuka jangwa.
Kufuatia
hali hiyo Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wawachukulie hatua watu wote
watakaokutwa wakiendesha shughuli mbalimbali kama za kilimo, ujenzi wa
makazi na uchungaji wa mifugo ndani ya vyanzo vya maji kwa kuwa
zinasababisha ukame.
Awali
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Lwenge aliwaagiza Wakandarasi
wanaojenga mradi huo kuhakikisha wanajenga kwa kuzingatia viwango vya
ubora vinavyohitajika pamoja na kumaliza kwa wakati. Mradi huo
unatarajiwa kukamilika Julai, 2018.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, SEPTEMBA 21, 2017.
No comments:
Post a Comment