Baadhi
ya wabunge wa mabunge ya Uingereza wakiwa katika kikao na Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt, Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani),
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa tatu
kushoto), akiongoza majadiliano na Ujumbe wa Wabunge watano pamoja na
maafisa kadhaa kutoka nchini Uingereza, walipomtembela na kufanya naye
mazungumzo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto),
akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungungumzo na wabunge kutoka
nchini Uingereza waliomtembelea Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni
Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta
Mutagwaba.
Baadhi
ya Ujumbe kutoka Tanzania walioshiriki mazungumzo kati ya Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na baadhi ya Wabunge
kutoka nchini Uingereza, Jijini Dar es Salaam (kulia ni Mkurugenzi wa
masuala ya Sheria Bi. Susana Mkapa akifuatiwa na Kaimu Katibu Mtendaji
wa Tume ya Mipango Bw. Paul Sangawe.
Kamisha
wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Mgonya Benedicto (kushoto) na
Msajili wa Hazina, Dkt. Oswald Mashindano, wakifuatilia kwa makini
mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb) na wageni wake, Wabunge wa Mabunge ya Uingereza (Baraza la
Mamwinyi na Bunge la Wawakilishi).
Kiongozi
wa Wabunge wa Bunge la Uingereza waliotembelea nchini na kufanya
mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb), Mhe. David Linden, akizungumza namna nchi hiyo inavyosaidia
masuala mbalimbali nchini ikiwemo Elimu na lishe.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia),
akizungumza na Wabunge kutoka Nchini Uingereza waliomtembelea katika
Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja
na kuipongeza nchi hiyo kwa kuisadia Tanzania katika masuala mbalimbali,
amesisitiza ushirikiano wa nchi hizo mbili ujikite zaidi katika masuala
ya biashara na uwekezaji.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili
kushoto) na Kiongozi wa Ujumbe wa Wabunge kutoka Uingereza, Mhe. David
Linden (katikati) na Wabunge wengine kutoka Uingereza, Maafisa
Waandamizi kutoka Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya
kumalizika kwa Mkutano katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)
(katikati)akijadili jambo na baadhi ya maafisa walioambatana na Wabunge
wa Bunge la Uingereza baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao
ulioangazia utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka
Mitano, Elimu, lishe, na Matumizi adili ya rasilimali fedha, Mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Tanzania
imetoa rai kwa Serikali ya Uingereza kubadili mfumo wa uhusiano wake
kwa kujikita zaidi katika masuala ya biashara na uwekezaji badala ya
kutoa misaada ya kawaida ili nchi iweze kukuza uchumi wake kwa haraka
zaidi.
Wito
huo umetolewa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Philip Isdor Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa
wabunge kutoka mabunge ya uingereza (Baraza la Mamwinyi na Bunge la
Wawakilishi).
Dokta
Mpango amesema kuwa kiwango cha mtaji ambacho Serikali ya Uingereza
imewekeza nchini hadi sasa ni Paundi bilioni 2.5 lakini kwa upande wa
biashara kati ya nchi hizo mbili, hali si nzuri.
"Mwaka
2015 Tanzania iliuza nje bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani
milioni 22.5 na kununua bidhaa kutoka Uingereza zenye thamani ya Dola
milioni 150, kiwango ambacho ni kidogo sana na tunahitaji kufanya
biashara zaidi" Alisisitiza Dkt. Mpango.
Alielezea
hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua kuimarisha uchumi wa
viwanda na kuelezea changamoto kubwa ikiwa na namna ya kuendeleza kilimo
kwa ajili ya kupata malighafi za viwanda na kuwainua wananchi kiuchumi
kwa kuwa kilimo ndicho kinaajiri idadi kubwa ya Watanzania.
Dkt.
Mpango alitoa wito kwa Serikali ya Uingereza kuwekeza zaidi katika
viwanda vitakavyoongeza thamani ya bidhaa mbalimbali ikiwemo kujenga
viwanda vya kutengeneza matrekta na zana nyingine za kilimo, kusindika
bidhaa za mazao ya wakulima pamoja na kuwekeza katika sekta za kuongeza
thamani ya madini na nishati ya umeme.
Dokta
Mpango aliwaeleza Wabunge hao kwamba hivi sasa Serikali imepiga hatua
kubwa kiuchumi na kuishukuru Uingereza kwa mchango mkubwa inaoutoa
kusaidia Elimu, Lishe, Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma na afya
kwa upande wa lishe, uwekezaji ambao kwa pamoja umefikia zaidi ya paundi
milioni 180.
Kwa
upande wake, kiongozi wa Wabunge watano waliomtembelea Waziri wa Fedha
na Mipango, Mheshimiwa David Linden, amesema wamefurahishwa na namna
Tanzania inavyopiga hatua kubwa kimaendeleo na kudhibiti vitendo vya
rushwa.
Amesema
kuwa wameridhishwa na kiwango cha miradi wanayoifadhili katika sekta ya
elimu na afya hususan masuala ya lishe kwa watoto na kwamba nchi yao
itaendelea kuisaidia Tanzania ili iweze kufikia malengo yake kiuchumi na
kijamii
No comments:
Post a Comment