![]() |
| Wajumbe
wa mkutano wa ushuri wa kisaikolojia kwa watoto wakifatilia mada katika
mkutano wa siku tatu jijni Arusha ulioandaliwa na taasisi ya
REPSSI. |
![]() | ||
| Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo. |
Filbert Rweyemamu,Arusha.
Serikali
imesema licha ya jitihada inazofanya kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali bado zipo changamoto zinazowakabili watoto nchini hivyo
imeanda mpango wa kitaifa utakaotumika kuwalinda watoto dhidi ya vitendo
vya ukatili.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto,Hamisi Kigwangalla wakati akifungua mkutano wa siku tatu
ulioandaliwa na taasisi ya REPSSI inayojihusisha na ushauri wa
kisaikolojia na malezi kwa watoto katika nchi za Kusini na Mashariki mwa
Afrika.
Alisema
kupitia taasisi zake iliandaa mikakati nane ambayo hadi mwaka
walikubaliana kuinganisha mikakati hiyo ili kupata mpango mmoja wa
kitaifa ambao unazuia vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
"Katika
mpango huo tunaeleza majukumu ya kila taasisi za serikali,binafsi na
taasisi za kimataifa zinazojihusisha na kupiga vita vitendo vya ukatili
dhidi ya watoto ndio utakaotumika katika kipindi cha mwaka 2017 hadi
2022 ili tumbunguze vitendo hivi kwa asilimia 50,"alisema Kingwangalla
Aliongeza
kuwa mpango huo umeongeza adhabu kwa watakaobainika kuwafanyia watoto
vitendo vya ukatili na umekusudia kujenga mahusiano ya karibu na taasisi
zote ili kurahisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wanaopatikana
na makosa hayo.
Dk
Kigwangalla alisema hapa nchi takwimu za mwaka 2009 za utafiti
zinaonesha kati ya watoto watatu wa kike mmoja amefanyiwa vitendo vya
ukatili wa ngono akiwa chini ya miaka 18 wakati kati ya watoto saba
mmoja amefanyiwa ukatili wa kijinsia.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika(EAC)Balozi Liberat
Mfumukeko alisema watoto na vijana katika nchi za jumuiya wanafikia
asilimia 50 lakiniwanakabiliwa na migogoro ya kivita,Ukimwi,ukutili wa
kingono,matendo ya udhalilishaji,ukahaba katika umri mdogo na umasikini.
Alisema
kama jumuiya imeweka utaratibu wa kuwalinda watoto kwa kuanzisha baraza
la kanda linalojihusisha na jinsia,vijana,watoto,maendeleo ya jamii na
ulinzi kwa lengo la kuhakikisha nchi wanachama wanazingatia mpango
pamoja ile iliyo katika nchi zao.
Naye
Mkurugenzi wa REPSSI hapa nchini,Edwick Maphalala amesema jamii nzima
inao wajibu wa kujenga mazingira mazuri ya kuhakikisha haki za watoto
zinalindwa na inapotokea watoto wameathirika na matatizo ya mapigano
wanatakiwa kupewa ushauri wa kisaikolojia.
Mkutano
huo ni saba kufanyika tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo miaka 15
iliyopita na imeweza kuwakutanisha watoto kutoka mataifa 31.




Post a Comment