Na HAMZA TEMBA - WMU
-----------------------------------------------------------
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameliagiza Shirika la
Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Hifadhi ya Taifa ya Arusha
kuhakikisha kuwa wananchi wote waliolima ndani ya eneo la hifadhi hiyo
kinyume cha sheria wanaondoa mazao yao pamoja na kusitisha kabisa
shughuli zozote za kibinadamu ndani ya hifadhi hiyo.
Prof.
Maghembe ametoa agizo hilo jana wakati akiwa kwenye ziara yake ya
kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo iliyopo wilaya ya Arumeru mkoani
Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na hifadhi
hiyo ikiwemo maeneo yenye mgogoro kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi.
"Naagiza,
kuanzia leo ni marufuku mtu yeyote kuonekana akilima katika eneo hili,
wekeni askari hapa, atakayeonekana piga pingu, hatuwezi kushuhudia watu
wanalima ndani ya hifadhi tukae kimya, ni lazima tuchukue hatua.
Watangaziwe na wapewe muda wa kuondoa mazao yao, ndani ya siku 30 au 40
wawe wameshaondoka", alisisitiza Prof. Maghembe baada ya kukagua eneo
hilo.
Awali
akiwasilisha taarifa ya hifadhi hiyo kwa Waziri Maghembe, Mhifadhi Mkuu
wa hifadhi hiyo, Steria Ndaga alisema eneo hilo ambalo pia linajulikana
kama shamba namba 40 na 41 limekuwa na mgogoro tangu mwaka 1990 baada
wananchi wa Kijiji cha Olkung'wado kuvamia eneo hilo huku wakitoa hoja
kadhaa ikiwemo madai kuwa shamba hilo ni maeneo yao ya asili waliyokuwa
wakimiliki tangu zamani.
Alisema
hoja nyingine wanazozitoa ni kuwa walipewa mashamba hayo na Serikali
wakati wa operesheni ya uanzishwaji wa vijiji mwaka 1975 na 1976, Aidha,
hoja nyingine ni kuwa hawakushirikishwa kwenye mchakato wakati wa
ugawaji wa mashamba hayo na kwamba TANAPA pia haina hati miliki ya
mashamba hayo.
Ngada
alisema hoja zote hizo zilikinzana na ukweli ya kwamba shamba hilo
lilimilikishwa kwa TANAPA tangu mwaka 1980 baada ya kutolewa tangazo kwa
wadau wanaoweza kuliendeleza kufuatia muwekezaji wa awali, James
Preston Mallory kushindwa kuliendeleza na hivyo kufutiwa hati miliki na
Mhe. Rais mnamo mwaka 1979.
“Wadau
mbalimbali waliomba umiliki wake ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la
Ngorongoro na Halmashauri ya Kijiji cha Olkung'wado, lakini Kamati ya
Ushauri ya Ardhi ya Mkoa wa Arusha ikaishauri Serikali mashamba hayo
yamilikiwe na TANAPA na hivyo tukaandikiwa barua rasmi ya kukubaliwa
kupewa shamba na Idara ya Ardhi Mkoa” alisema Ndaga.
Alisema
TANAPA ilinunua eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 966 kwa lengo la
kupanua hifadhi ya Taifa ya Arusha ambapo baada kupewa shamba hilo,
iliagizwa kulipa fidia ya mali zilizokuwepo, mwaka 1983 tathmini
ikafanyika na malipo yakalipwa Serikalini hatimaye TANAPA ikapewa barua
ya kumiliki ardhi mwaka 1988. Alisema kwa upande wa Kijiji hicho
cha Olkung'wado hakuna nyaraka yeyote inayoonesha shamba hilo kupewa
kijiji hicho.
Mhifadhi
huyo alisema baada ya mgogoro wa muda mrefu, wataalam wa TANAPA
walifanya survey katika shamba hilo ili kubaini maeneo yaliyo na
shughuli nyingi za kibinadamu na yale yenye umuhimu zaidi kiikolojia,
mapendekezo yalitolewa kuwa maeneo yenye shughuli nyingi za kibinadamu
yaachwe kwa wananchi na yale yenye umuhimu kiikolojia yaendelee
kuhifadhiwa, Bodi ya TANAPA iliridhia ekari 366 zipewe wananchi na ekari
600 ziendelee kuhifadhiwa.
“Baada
ya kikao cha wadau wa uhifadhi kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru tarehe 11 Mei, 2017 ambacho kilijumuisha Madiwani, mwakilishi wa
Mbunge, katibu tarafa, watendaji wa kata, wenyeviti na watendaji wa
vijiji, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na wataalam wa
halmashauri, ilifikiwa maazimio ambapo wajumbe waliridhia maamuzi ya
Bodi ya Wadhamini ya TANAPA kuwapa wananchi ekari 366 ya shamba hilo na
kubakiwa na ekari 600” alisema Ndaga.
Aliongeza
“Kikao hicho pia kiliridhia TANAPA kuweka vigingi vya mpaka katika
shamba hilo ambapo tarehe 14 Mei, mwaka huu, 2017 zoezi hilo lilianza na
jumla ya vigingi 26 viliwekwa”.
Alisema
hata hivyo kumekuwepo na taarifa kuwa baadhi ya wanakijiji wa Kitongoji
cha Momella walifungua kesi mahakamani wakidai wakidai kuwa kijiji cha
Olkung'wado kimenyang'anywa ardhi yao na TANAPA, hata hivyo Serikali
hiyo ya Kijiji imekana kwa maandishi kuhisika na ufunguzi wa kesi hiyo
wakidai imefunguliwa na mtu binafsi na sio Serikali ya Kijiji hicho.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Alan Kijazi alimuhakikishia
Waziri Maghembe kuwa maagizo yote aliyoyatoa ya kusitisha shughuli za
kibinadamu ndani ya eneo hilo yatafanyiwa kazi na atapewa mrejesho wa
utekelezaji wake.
Hifadhi ya Taifa ya Arusha ilianzishwa mwaka 1960 wakati huo ikiitwa Ngurdoto na ina ukubwa wa kilomita za mraba 322. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa utalii wa magari, kutembea kwa miguu, kupanda milima (mlima Meru), utalii wa farasi, mitumbwi ya kuogelea, baiskeli na wa utalii wa kutumia farasi. Katika mwaka wa fedha uliopita 2016/2017 hifadhi hiyo ilivunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 12 ambapo ilikusanya Shilingi bil. 5.4.
Hifadhi ya Taifa ya Arusha ilianzishwa mwaka 1960 wakati huo ikiitwa Ngurdoto na ina ukubwa wa kilomita za mraba 322. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa utalii wa magari, kutembea kwa miguu, kupanda milima (mlima Meru), utalii wa farasi, mitumbwi ya kuogelea, baiskeli na wa utalii wa kutumia farasi. Katika mwaka wa fedha uliopita 2016/2017 hifadhi hiyo ilivunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 12 ambapo ilikusanya Shilingi bil. 5.4.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akiingia kwenye ofisi
kuu ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha jana Mkoani Arusha katika ziara yake
ya kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo iliyolenga kukagua shughuli
za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia
ufumbuzi. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Alan Kijazi.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisalimiana na Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha, Steria Ndaga alipowasili katika
ofisi kuu ya hifadhi hiyo jana Mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya
kikazi ya siku moja iliyolenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan
maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha, Steria Ndaga (wa pili kulia)
akiwasilisha taarifa ya hifadhi hiyo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii,
Prof. Jumanne Maghembe wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja
katika hifadhi hiyo jana ambayo ililenga kukagua shughuli za uhifadhi
hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi.
Prof. Maghembe akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA, Dkt. Alan Kijazi (kushoto) akizungumza kutambulisha
viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha kwa Waziri wa Maliasili, Prof.
Jumanne Maghembe (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja
katika hifadhi hiyo jana Mkoani Arusha ambapo ililenga kukagua shughuli
za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia
ufumbuzi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) na wajumbe wa
kikao hicho wakifuatilia taarifa kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Arusha
ambayo iliwasilishwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akiongea na viongozi wa
TANAPA kuhusu eneo lililolimwa na wananchi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Arusha kinyume cha sheria wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja
katika hifadhi hiyo iliyolenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan
maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi, aliagiza
wananchi hao waondolewe ndani ya siku 40. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
TANAPA, Dkt. Alan Kijazi na Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Steria Ndaga
(kulia).
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia)
akisikiliza ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Arusha, Steria Ndaga (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi
ya siku moja katika hifadhi hiyo jana ambayo ililenga kukagua shughuli
za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia
ufumbuzi.
Baadhi ya wanyamapori (Twiga na Pundamilia) wakionekana wakijivinjari ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe katika
hifadhi hiyo jana ambayo ililenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan
maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi.

إرسال تعليق