Afisa
afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na
viongozi wa vijiji wa tarafa ya pawaga kuhusu uboreshaji wa vyoo bora
kwa lengo la kutatua tatizo la ugonjwa wa kipindupindu ambalo limekuwa
likijitokeza mara kwa mara katika tarafa hiyo walianza kutoa elimu kwa
viongozi wote na baadae wakahamia kwa wananchi.
Afisa
afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akizungumza na mama
moja ambaye hana choo bora na kutundikiwa bendera ilikuwa inamuonyesha
kuwa hana choo bora katika kijiji cha mboliboli tarafa ya pawaga mkoani
Iringa.
Afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya akisimamia zoezi la utundikaji wa bendera kwa wasio na vyoo bora
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Halmashauri
ya wilaya ya Iringa imetumia shilingi milioni mia moja na tisini
(190,000,000 ) kupambana na tatizo la milipuko ya ugonjwa wa
kipindupindu katika tarafa ya pawaga na Idodi mkoani Iringa na ni
miongoni mwa halmashauri 156 zinazotekeleza kampeni ya kitaifa ya usafi
wa mazingira Tanzania bara.
Akizungumza
wakati wa utoaji elimu ya matumizi ya vyoo bora katika tarafa ya pawaga
afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Samwel Nkya aliwataka
wananchi kuanza kutumia vyoo bora ili kumaliza tatizo la milipuko ya
ugonjwa wa kipindupindu ambao umekuwa ukiwakumba mara kwa mara.
“Jamani
chanzo mmoja wapo cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ni matumizi ya
vyoo ambavyo sio bora hivyo mnatakiwa kutumia vyoo bora na kutoa elimu
kwa wananchi wenu maana nyinyi ndi wenye wananchi na leo tunawapa hii
elimu nyie viongozi tunaomba muifikishe elimu kwa wananchi”alisema Nkya
Nkya
alisema walitoa elimu ya uboreshaji wa miundombinu ya vyoo na kunawa
mikono kwa kutumia maji tiririka kwa sabuni mara ya kutoka chooni kwa
ngazi ya kaya na shule za msingi na sekondari,Vyuo,taasisi za
kidini,taasisi binafsi,taasisi za kiserikali kama ofisi za serikali na
vituo vya afya lengo likiwa ni kutokomeza kabisa ugonjwa wa
kipindupindu.
“Ukiangalia
hadi sana tumefanikiwa kuzifikia jumla ya kaya 24 zilizotekeleza
kampeni hiikupitia wadau mbalimbali kama wizara ya afya,wizara ya
maji,wizara ya elimu (RWSSP),halmashauri ya wilaya ya Iringa,UNICEFU,SNV
na WARID na jumla ya kata nne ambazo ni ilolompya,Mlenge,Mboliboli na
Itunundu zimeanza kutekeleza rasmi kampeni hii kwa mwaka wa fedha wa
2017/2018” alisema Nkya
Mwezi
wa pili hadi mwezi wan ne mwaka 2016 ndio kulitokea mlipuko wa ugonjwa
wa kipindupindu katika halmashauri ya wilaya ya Iringa ambapo kata za
Mboliboli na Mlenge zilikumbwa na ugonjwa huo huku vijiji vya
Luganga,Mnadani,Idodi na Mafuruto vilikuwa na idadi ndogo ya wagonjwa wa
kipindupindu.
Aidha
Nkya alisema kuwa mikakati ya halmashauri ya wilaya ya Iringa kuzitambua
kaya na taasisi zisizo na vyoo bora,kutambua vibarua na wamiliki wa
mshamba ya mpunga,kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa usafi wa mazingira
vijijini na kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa ajili ya kujikinga na
ugonjwa wa kipindupindu kisitokee tena katika halmashauri hiyo.
“Tumepeana
maagizo ya kutekeleza kama kuwawekea bendera nyekundu kaya na taasisi
zote ambazo hazina vyoo bora,kutoa muda maalumu wa kuboresha vyoo vyao
vinginevyo kuna faini ambayo itatolewa kwa kaya na taasisi ambazo
zitakuwa hazijaboresha vyoo vyao” alisema Nkya
Nyamiki
Kimsau ni mwananchi wa kijiji cha Usolanga pawaga alisema kuwa kuwa
ugonjwa kipindupindu umekuwa sugu katika kijiji hicho kutokana na
wananchi wemgi kutokuwa na vyoo bora ambavyo vinakidhi kuishi na afya
bora.
“Wananchi
tukiwa tunafanya usafi na kuwa na vyoo bora basi tunaweza kuepukana na
milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu hivyo naomba serikali kuwa wakali
kwenye swala la kuwa na vyoo bora ili kuondokana na aibu ambayo imekuwa
inatutafuna kwa muda sasa” alisema Kimsau
Naye
Mwaita Bin jumbe alisema kuwa kweli wananchi wa kijiji cha mboliboli
hawana vyoo bora kutokana na ugumu wa maisha hivyo wanaomba kupewa muda
ili waweze kuboresha vyoo bora lakini swala la ugonjwa wa kipindupindu
bado unawakumba kila mara.
“Jamani
tunaomba viongozi mtoe elimu ya kutosha kwa wananchi ili wajue umuhimu
wa kuwa na vyoo bora tofauti na hali iliyopo hivi sasa” alisema Bin
jumbe
Hamis
Matyame ni kijana wa kijiji cha mboliboli aliita serikali ya kijiji
kutafuta njia mbadala ya kuwachimbia vyoo bora wazee ambao hawana uwezo
wa kifedha na guvu kazi kwa sababu wasipo saidiwa ugonjwa wa
kipindupindu hauta koma katika tarafa ya pawaga.
“Mimi
kama kijana napenda kuwasaidia wazee kuboresha vyoo ila hapa kijijini
kuna wazee wengi hivyo pekee yangu siwezi hivyo naiomba serikali
kutafuta njia mbadala kuwasaidia hawa wazee” alisema Matyame


Post a Comment