|
Baadhi
ya Washiriki walioshiriki kikao cha kikao cha Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini
Dodoma leo
Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Eng. Musa Iyombe amesema Serikali
itahakikisha inatekeleza maazimio yote
yaliyopitishwa kwenye Mkutano wa pamoja wa mwaka wa wadau wa Elimu uliofanyika kwa
siku nne Mjini Dodoma.
Eng. Iyombe ameyasema
hayo wakati wa kufunga Mkutano wa mwaka wa wadau wa Elimu wenye lengo la
kujadili changamoto, mafanikio ya Elimu na kuona namna gani kama wadau wanaweza
kutafuta njia ya pamoja ya kuboresha Mfumo wa utoaji wa Elimu Tanzania.
“Nimepokea maazimio yote
ya Mkutano huu na ntayawasilisha
panopohuiska kwa ajili ya Utekelezaji lakini pia niwapongeze kwa kazi kubwa
mliofanya, kuanzia wataalamu kutoka Serikalini, sekta binafsi, Mashirika yasiyo
ya kiserikali, wadau wa Elimu hakika mmefanya kazi kubwa na kupitia Mkutano huu
tutaona mabadiliko makubwa katika Sekta hii ya Elimu” alisema Iyombe.
Akitoa salamu za
Wizara Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu Sayansi na Teknolojia Prof sylivia Temu amesema Kikao kimekuwa na tija
kwa kuwa pamoja na mambo mengine kimejadili masuala yanayotokana na utafiti wa
elimu na kwamba matokeo ya tafiti yaliyoonyesha changamoto yatafanyiwa kazi kwa pamoja kati ya
serikali, wadau wa maendeleo na mashirika yasiyo ya serikali.
|
إرسال تعليق