Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito
Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa
Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya,
katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar
es Salaam Agosti 25, 2017.
Wahandisi
wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya
kuibuka wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha
wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama
"Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE".
Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia
teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme
(Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito
Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo,
kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili
wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye
waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.
Dkt.
Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam,
wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa
tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi
wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition,
(TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi
lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
“Niwapongeze
sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini
niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi
wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia
kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo
baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt.
Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga
picha (image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia
wateja wetu. Alisema.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica
Lutenganya, alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha
umahiri wao katika kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya
usambazaji umeme (Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha
huduma wanazozitoa katika jamii.
“Lakini
pia si hivyo tu, tulionyesha uboreshaji wa huduma tunazozitoa kwa
wateja kwa kutumia teknolojia ya kisasa kupitia mfumo wa fiber ambao
upitishaji taarifa mbalimbali kama vile mawasiliano na picha na hii
inawezesha mfumo kuliona tatizo la mteja mara tu linapotokea na
kuwezesha TANESCO kuchukua hatua haraka bila mteja kupata usumbufu.”
Alisema Mhandisi Lutenganya.
Katika
Kongamano hilo la mwaka huu lililofanyika Julai 28, (2017), kulikuwa na
makundi matatu ya washiriki, ambayo ni shule za Sekondari, taasisi za
elimu ya juu na mashirika ya umma ambapo waandaaji waliangalia uandaaji,
uelewa wa washiriki pamoja na teknolojia ilivyotumika.
TANESCO ina wahandisi wanawake 55, na kuifanya taasisi ya kwanza nchini kuwa na idadi kubwa na wahandisi wanawake.
Naye
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na
huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, alisema ni wajibu wa
wanawake kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yao na kuachana na
dhana ya woga.
“Fanyeni
kazi kwa bidii na maarifa, na niwaambie, utendaji kazi wako ndio
utamvutia MD afikie uamuzi wa kukupandisha cheo na sio jambo linguine
lolote lile, mimi nitastaafu hivi karibuni, ninawaeleza haya kwavile
ninajua umuhimu wa kujituma katika kazi na kujiamini.” Alisema Mhandisi
Ngahyoma.Alionyesha kufurahishwa kwake, na angependa idadi ya wanawake
viongozi katika Shirika hilo inaongezeka na kufikia sio asilimia 50 tu
bali asilimia 75.
Naibu
Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa
wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akiwa na Dkt. Mwinuka wakati
akionyesha tuzo hiyo.
Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Naibu
Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa
wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, akizungumza.
Naibu
Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa
wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.













إرسال تعليق