|
SHIRIKA la Posta na Simu chini ya uongozi mpya, imejinyakulia tuzo ya mshindi wa kwanza wa
watoa huduma bora kutoka taasisi za umma na binafsi, zinazoshiriki maonesho ya
41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, yaliyofunguliwa rasmi na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Julai 1, 2017.
Maonesho hayo ya kila mwaka yameandaliwa na Mamlaka ya Uendelezaji Bishara
Tanzania, (TAN Trade). Pichani juu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania,
Bw. Deo Kwiyukwa, (katikati), akiwa amekamata tuzo hiyo pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo kwenye banda lao. |
|
Bw. Kwiyukwa (kushoto), akiwakabidhi tuzo hiyo wafanyakazi wenzake baada ya kupokea toka kwa Rais Magufuli. |
Wafanyaakzi wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwahudumia wananchi waliotembelea banda la shirika hilo kwenye banda kuu la Jakaya Kikwete.
Wafanyaakzi wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwahudumia
wananchi waliotembelea banda la shirika hilo kwenye banda kuu la Jakaya
Kikwete.
|
Bw. Kwiyukwa, (Kushoto),
akifurahia jambo na Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano na elimu kwa
umma, wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi. Sara
Kibonde Msika, (kulia), na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano
wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Laura Kunenge. |
|
Bw. Kwiyuka akipongezwa na Bi Laura Kunenge wa WCF, baada ya kutwaa tuzo hiyo |
No comments:
Post a Comment