Na Christina Mwangosi, MOHA
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dk. Juma Malewa amesema Jeshi la
Magereza nchini litatoa elimu ya namna kila Mtanzania hata aishie kwenye
nyumba za ghorofa ama maeneo yenye nafasi ndogo ya kuanzisha kilimo cha
mbogamboga, anavyoweza kutumia eneo dogo kuendeshea shughuli za kilimo
cha mbogamboga wakati huu Maonyesho ya SabaSaba yanayoendelea katika
Viwanja vya SabaSaba jijini Dar es salaam.
Kamishna
Jenerali Dk. Malewa amesema kuwa pamoja na kuandaa Shamba Darasa kwa
ajili ya kutoa elimu ya shughuli mbalimbali za kilimo, Jeshi la Magereza
limeandaa bidhaa mbalimbali ambazo zitaonyeshwa wakati wote wa
Maonyesho pamoja na kuuzwa wakati wote wa Maonyesho hayo.
Dk.
Malewa amesema miongoni mwa bidhaa hizo ambazo ziko kwenye Banda la
Magereza ni samani mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi na nyumbani
ikiwemo makabati ya vyombo na nguo, meza na viti, madawati kwa ajili ya
shule za msingi na sekondari, vitanda, sofa, ‘dressing table’ pamoja na
viatu vya ngozi vya kike na kiume.
Amesema
Jeshi la Magereza pia litauza pia majiko sanifu yanayotumia kuni kidogo,
mashuka, foronya, vikoi pamoja na sabuni zenye ubora kwa ajili ya kufua
nguo ambazo zinatengenezwa katika Kiwanda cha Sabuni kilichopo Mkoa wa
Mbeya.
Amesema
Jeshi la Magereza katika kipindi hiki cha Maonyesho litatoa elimu ya
shughuli za kilimo cha kisasa bure na kwa wale wananchi ambao maeneo yao
yanafikika Wataalamu wa Magereza wanaweza kuwatembelea wananchi kwenye
maeneo yao na kuwafundisha namna ya kuanzisha kilimo hicho
kinachojulikana kama ‘kilimo cha jikoni’.
No comments:
Post a Comment