Pages

July 7, 2017

Rejista ya Wahisiwa kuwa na Kifua Kikuu(TB) yazinduliwa Mjini Dodoma

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikari za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akikata utembe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Rejista mpya ya wanaohisiwa kuwa na Kifua kikuu ambayo itaanza kutumika kwenye vituo vyote vya kutolea huduma, wakati wa Mkutano wa mwaka wa Waganga waWakuu wa Mikoa na Wilaya unaoendelea Mjini Dodoma,Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangwalla
Dkt.Hamisi Kigwangwalla akisoma moja ya Rejista hiyo ambayo imezinduliwa rasmi leo,kulia kwake ni Waziri Simbachawane na aliyesimama kushoto ni Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu Chaula
Waziri Simbachawene akimkabidhi Rejista hiyo Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI upande wa Afya Dkt. Zainabu Chaula
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athumani Masasi wakipeana Rejista hiyo na Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Mikoa ambaye ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt. Leonald Subi(kulia)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athumani Masasi akiwa na Mkurugenzi toka Global Fund-Geneva Dkt.Osamu Kunii mara baada ya Kukabidhiwa Rejista hiyo na Waziri Simbachawene

Baadhi ya Wakurugenzi toka Wizara ya Afya,TAMISEMI pamoja na Taasisi za Wizara ya Afya wakitambulishwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya unaofanyika kwenye ukumbi wa LAPF Mjini Dodoma(Picha zote na Wizara ya Afya)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...