Msanii
wa Bongo flava na mfalme wa miduara AT, akiongelea utamaduni wa
kiswahili na raha za pwani kwenye jopo la kongamano la raha za pwani kwa
lengo la kudumisha na kutangaza utamaduni wa Mswahili na lugha yake.na
baadae kuonesha onesho kali ya nyimbo zake zilizotamba na zinazoendelea
kutamba kwenye anga ya bongo na kimataifa. Kongamano hilo linaloambatana
na tamasha la Mswahili na lugha yake huandaliwa na Swahili Media
Network na hufanyika mara moja kila mwezi. Picha na Vijimambo Blog na
Kwanza Production.
Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT akichengua mashabiki wake kwa wimbo mmoja wapo wa mduara.
Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT usipime ni balaa
Msanii
wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa buradani kwenye jopo la kongamano la raha
za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 Hampton Inn,
College Park, Maryland.
Msanii wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa buradani kwenye jopo la kongamano la raha za pwani
Aisha
akifungua pazia kwenye jopo la kongamano la raha za pwani kwa lengo la
kudumisha na kutangaza utamaduni wa Mswahili na lugha yake.na baadae
kumkaribisha mratibu wake Bwn. Mgaza (hayupo pichani).
Mratibu
wa Raha za Pwani Bwn. Mgaza akiuelezea Utamaduni wa Kiswahili na lugha
yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya
Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.
Bi
Rukia akichangia nini maana ya Utamaduni wa Kiswahili na lugha yake
kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi
July 22, 2017 College Park, Maryland na huku akitoa rai kwa wazazi
ughaibuni kuacha kudharau utamaduni wa wetu na wafanye kazi ya ziada
kuwafundisha watoto wa ughaibuni lugha ya Kiswahili na utamaduni wake.
Mama
mitindo na mkurugenzi wa Miss Tanzania USA MaWiny Casey akichangia vazi
la khanga na utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la
kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017
College Park, Maryland.
Mama
mitindo na mkurugenzi wa Miss Tanzania USA MaWiny Casey akimkabidhi
tuzo Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza linalosimamia shughuli za utamaduni
na Sanaa nchini Tanzania (BASATA) - Bwana GODFREY LEBEJO MNGEREZA,
aliefuatana na Msanii maarufu wa nyimbo na ngoma ya Muduara- Bwana ALI
RAMADHAN ALI, al-maarufu kwa jina la MR. AT kwenye jopo la kongamano la
raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park,
Maryland.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Baraza linalosimamia shughuli za utamaduni na Sanaa nchini
Tanzania (BASATA) - Bwana GODFREY LEBEJO MNGEREZA akiongelea muziki
unavyodumisha utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la
kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017
College Park, Maryland.
Watoto
Imani (kushoto)naAaliyah wakicheza moja ya mchezo ya watoto
wanavyocheza kwa Kiswahili kama moja ya kudumisha Kiswahili na utamaduni
wake.
No comments:
Post a Comment