Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi),George Simbachawene akiwasalimia wananfunzi wa Shule ya Sekondari Chinyika wakati wa ziara yake jimboni Kibakwe |
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais (Tamisemi),George Simbachawene(kulia) akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka
kwa wananchi wa Kijiji cha Fufu alipofanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Tamisemi),George Simbachawene(kulia)katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Fufu.
|
Nteghenjwa
Hosseah, Kibakwe
Imekua ni hulka
inayoendelea kukua katika Halmashauri nyingi nchini kuanzisha miradi mipya
ilihali miradi viporo ikiendelea kuzorota kwa miaka kadha wa kadha bila kukamilika huku ikiharibika na kusababisha
upotevu wa Fedha zilizowekwa hapo awali.
Hali hii imebainika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakati
wa ziara ya kikazi ya Mhe. Waziri wa Nchi ofisi ya Raisi Mhe. George
Simbachawene alipotembelea kijiji cha Chinyika Kata ya Mlunduzi, Tarafa ya Rudi
iliyopo Katika Jimbo la Kibakwe na kukuta baadhi ya miradi kutokamilika
kutokana na kutotengewa Fedha katika Bajeti ya mwaka wa Fedha uliofuata.
Akizungumza na wananchi
wa Kijiji cha Chinika Mhe Simbachawene alisema ni vyema miradi inayofadhiliwa
na wadau na ile ya halmashauri kuwa na umiliki (ownership) na kuthamini nguvu
na fedha zilizotumika ili hata ikiishia katikati Halmashauri husika ama
wananchi wa eneo hilo kuwa na moyo wa
kuendelea kutenga fedha au kuchangia kutoka mifukoni mwenu na kukamilisha mradi
husika.
Unakuta Halmashauri
inatenga Fedha kidogo kwa ajili ya mradi Fulani na unaishia katikati kasha
mwaka unaofuata wa Fedha watengea miradi mipya badala ya kuhakikisha wanakamilisha
ule wa awali hii inasababisha mradi ule kuharibika kwa kukaa muda mrefu hivyo
fedha za Serikali kupotea bila manufaa yenye tija kwa wananchi alisema Mhe.
Simbachawene.
Kuna wakati wadau wanatoa fedha kutoka kwenye mapato yake na kuamua kutatua
changamoto lakini akiishia katikati basi wananchi na halmashauri hakuna
anayejishughulisha ili kupata fedha za kukamilisha mradi kila mtu anaona kama
hahusiki na ukamilishaji wa mradi huo hii si tabia nzuri na naikemea na
kuzitaka Halmashauri zote kuiacha mara moja aliongeza Simbachawene.
Alisisitiza kuwa wakati
Fulani Halmahsuri ilitoa Tsh Mil 26 kwa ajili ya nyumba ya mwalimu (Two in One) na fedha
hazikutosha: Nilitegemea Halmashauri wataingiza kwenye mpango wa bajeti mwaka
unaofuata lakini hamna kitu na mpaka leo jingo hilo halijakamilika.
"Natoa Agizo kwa
Halmashauri zote Tanzania kuhakikisha miradi yote iliyoanzishwa na wadau, nguvu
za wananchi au Serikali kuhakikisha inakamilika kabla ya kuanzisha miradi mipya
kupitia njia hii thamani ya fedha itaonekana, tofauti ya hapo fedha zilizotumika zitapotea
bila kusaidia jamii" Alisema Simbachawene.
Awali katika ziara hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir
Shekimweri aliwasilisha changamoto za wananchi wa Kijiji cha Chinyika kuwa
ni sintofahamu ya mapato ya Mnara wa Halotel ulisimikwa katika kijiji lakini
kijiji hakinufaiki na mapato, baadhi ya wananchi kushiriki kwenye Kilimo
cha Bangi na Wakazi wachache kuharibu chanzo cha maji hivyo kusababisha ukosefu
wa Maji kwa wananchi wote wa kijiji cha Chinyika.
Mhe.Simbachawene
ameahidi kuongeza nguvu katika operesheni ya kuwakamata wale wote wanaolima
Bangi katika Jimbo la Kibakwe na kuwapeleka Mahakamni yeyote atakayekamatwa
kuharibu chanzo cha Maji.
Mhe. Simbachawene
anaendelea na ziara yake katika Jimbo ka Kibakwe na katika siku ya pili
ametembelea vijiji vya Chinyika, Chaludewa pamoja na Fufu.
No comments:
Post a Comment