Pages

June 29, 2017

RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakati wa ziara yake wilayani humo. Wengine pichani kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa huo, Muliro Jumanne Muliro.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiangalia mashine za kukoboa na kusaga nafaka pamoja na kusindika alizeti kutoka mjasiriamali Mzee Nassoro alipokuwa kata ya Mwamamalasa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akiwa na Katibu Tawala Mkoa, Albert Msovela (katikati) pamoja na Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese (kushoto) wakati wa ziara.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga.
Mjasirimalia Mabela Msolwa kutoka wilayani Kishapu akitoa maelezo kuhusu mradi wake wa mashine za kuchakata nafaka na ghala kuhifdhi nafaka kwa Mkuu wa mkoa (kulia) na viongozi wengine wakati wa ziara hiyo.
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kishapu, Lucas Said (kushoto) akitoa maelezo kuhusu mradi wa huduma ya maji ya Ziwa Victoria kwa wananchi kata ya Maganzo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akitoa maelekezo wakati alipotembelea ghala la nafaka la Mabela mjini Mhunze kata ya Kishapu wakati wa ziara yake.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akifafanua jambo kwa viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo kijiji cha Kinampanda kata ya Mwamalasa.

Na Robert Hokororo

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika ziara hiyo Telack alikagua mradi wa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria uliopo kata ya Maganzo na maendeleo ya ujenzi wa zahanati kata ya Shagihilu.

Mradi mwingine ni wa mjasiriamali wa kusindika alizeti na kukoboa nafaka za mpunga na mahindi ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Kwenye kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea mradi mwingine wa ghala la kuhifadhi nafaka na mashine za kukoboa nafaka za mahindi na mpunga.

Katika ziara hiyo kiongozi huyo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa was Shinyanga, Muliro Jumanne Muliro.

Alikaribishwa na mwenyeji wake, Mkuu wa wilaya, Nyabaganga Talaba, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya na wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...