Na Chalila Kibuda, Dodoma
Vijana wengi wanaangamia kutokana na kutumia dawa za kulevya na kufanya taifa kukosa nguvu kazi ya kufanya uzalishaji.
Hayo
ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana wakati wa
uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani
yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square mkoani hapa, amesema
kuwa vijana kuwa na familia wameshindwa kuwa wazalishaji kwa kuishia
katika matumizi ya dawa za kulevya.
Amesema
vita ya dawa za kulevya ilishatangazwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli
na wengine ni kufanya utekelezaji kuhakikisha linafanikiwa dhidi vita ya
dawa za kulevya.
Rugimbana
amesema kuwa Dodoma inalengwa na kuwindwa kutokana na vyuo vingi kuwepo
hali ambayo vijana wanaweza kungeuka na kujiingiza katika matumizi ya
dawa za kulevya.
Katika
maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku matumizi ya shisha
katika hoteli zilizopo katika mkoa wake kutokana na kuwa sehemu ya dawa
za kulevya.
Aidha
amemuomba Mkurugenzi wa Life and Hope Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim
Bhanji kujenga sober house katika mkoa wa Dodoma kutokana na kuwepo kwa
kundi la vijana ambao wameathrika na matumizi ya dawa za kulevya.
Bhanji
amesema kuwa wanaangalia uwezo katika kuweza kujenga kituo ili kuweza
kuwarudisha vijana kutoka katika matumizi ya dawa za kulevya na kuwa
wazalishaji katika taifa lao.
Amesema
kuwa vijana wanaathirika sana na matumizi dawa za kulevya na kufanya
familia zao kuwa na mzigo wa kuwategemea wazazi wakati wazazi hao
walitakiwa kusaidiwa na vijana wao.
Katika maonesho hayo yameshirikisha umoja wa vituo vya kuhudumia walioathirika na dawa za kulevya Voice of Sober Houses (VOS).
Kamishina
wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga akipeana
mkono na Mkurugenzi wa Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim
Bhanji jana wakati maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya kupiga vita
dawa za kulevya Duniani katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma
Jana.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipeana mkono na Mkurugenzi wa
Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji wakati
alipotembelea banda la Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo katika
maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika
katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipata maelezo katika banda la
Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya kutoka kwa Mkaguzi wa Jeshi la
Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Anastazia Sauli katika
uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani
yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akizungumza na katika uzinduzi wa
maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika
katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma .
Kamishina
Msaidizi wa Idara ya Kinga , Tiba na Utafiti ,DK. Cassian Nyadindi
akitoa maelezo juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya katika
uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani
yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Wananchi
waktembelea mabanda mbambali juu ya huduma wanazozitoa katika uzinduzi
wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani
yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Picha ya pamoja.
Sehemu
ya wananchi wakiwa katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za
kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini
Dodoma.
No comments:
Post a Comment