MBUNGE
wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM) amepanga kutumia zaidi
ya Sh Milioni 60 kutoka katika mshahara wake kuwawezesha wanawake
katika kata 107 za mkoa wa Iringa kuanzisha mifuko maalumu ya
kuwezeshana kiuchumi.
Zaidi
ya kata 40 za wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi zimekwishanufaika na
mpango huo unaokiwezesha kikundi cha wanawake katika kila kata kupata Sh
600,000 ambazo hazirudishwi. Akikabidhi kiasi hicho cha fedha kwa
vikundi vya kata za Nyololo na Malangali, Tweve alisema zoezi hilo
litaendelea katika kata zingine zote zilizobaki zitakazokamilisha
taratibu mbalimbali ikiwemo ya kuunda uongozi wake na kufungua akaunti
benki.
Tweve
alisema kwa kupitia mifuko hiyo itakayojulikana kama mifuko ya Rose
Tweve ya kila kata wanawake watajiwekea utaratibu wa kuweka na kukopa,
kuinuana kimaendeleo na kubuni mambo mengine yatakayowazidishia kasi ya
maendeleo yao. “Wanawake tupo wengi sana, lakini tunakabiliwa na
changamoto mbalimbali zinazoturudisha nyuma. Huu ndio muda wa kujipanga
upya na kubadili maisha yetu kwa kutumia kauli mbiu ya rais wetu Dk John
Magufuli ya Hapa Kazi tu,” alisema.
Alisema
kutakuwepo na utaratibu wa kuvifanyia tathimini vikundi hivyo na vile
vitakavyofanya vizuri vitapata nyongeza ya fedha kila mwaka kwa kupitia
mpango huo na matokeo chanya yatakayojitokeza katika vikundi hivyo
yatamshawishi atafute wafadhili wengine wa ndani na nje ili wasaidie
zaidi.
“Nimeanzisha
mpango huu kwa kutumia rasilimali zangu mwenyewe na kwangu mimi naona
hili la kusaidia wanawake wenzangu kwa kutumia rasilimali zangu
linawezekana, sitoi fedha hizi ili mgawane kwa matumizi yasiofaa, natoa
kama jitihada zangu za kuwahamasisheni kuona haja ya kuwekeza kwa pamoja
na kwa manufaa ya wote,” alisema.
Akishukuru
kwa mchango huo, mmoja wa viongozi wa kikundi cha wanawake wa mfuko wa
Rose Tweve wa kata ya Malangali, Judith Kisinini alisema wako katika
mchakato wa kuanzisha duka la kuuza pembejeo za kilimo, hatua
itakayowawezesha wanawake wakulima wa kata hiyo kupata huduma hiyo kwa
gharama nafuu.
Kisinini
alisema kikundi chao chenye wanachama zaidi ya 200 hadi sasa
kimejiwekea taratibu mbalimbali za kufikia malengo yao na kila mwaka
kila mwanachama atalazimika kuchangia sh 50,000 kama hisa. “Fedha hizo
pamoja na michango ukiwemo wa mheshimiwa mbunge na faida tutakayokuwa
tunapata kutoka katika shughuli tutakazokubaliana kufanya zitatumika
kuendeleza wanachama wote bila ubaguzi wowote,” alisema.
Diwani
wa kata ya Malangali ambaye pia ni katibu wa mbunge huyo, Shakila Salim
aliunga mkono juhudi za mbunge huyo kwa kuvichangia vikundi hivyo Sh
100,000 kila kimoja na Tweve alikipongeza kikundi cha kata ya Mtitu
wilayani Kilolo ambacho mapema mwaka huu alikipatia kiasi hicho cha
fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wake ambao sasa una zaidi ya Sh
Milioni 1.8.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM) akizungumza na
wananchi wa kata ya Nyololo wakati wa muendelezo wa ziara yake kata 107
ya kuwahamisha wanawake wajiinue kiuchumi kwa kutumia vikundi pamoja na
kuwawezesha kwa kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa
ajili ya kujiendeleza.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM) akifurahi pamoja na
wananchi wa kata ya Nyololo wakati wa muendelezo wa ziara yake kata 107
ya kuwahamisha wanawake wajiinue kiuchumi kwa kutumia vikundi pamoja na
kuwawezesha kwa kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa
ajili ya kujiendeleza.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM) akizungumza na
wananchi wa kata ya Malangali wakati wa muendelezo wa ziara yake kata
107 ya kuwahamisha wanawake wajiinue kiuchumi kwa kutumia vikundi pamoja
na kuwawezesha kwa kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa
ajili ya kujiendeleza.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM akikabidhiwa zawadi ya
kitenge na wanawake wa kata ya Malangali Mkoa wa Iringa wakati wa
muendelezo wa ziara yake kata 107 ya kuwahamisha wanawake wajiinue
kiuchumi kwa kutumia vikundi pamoja na kuwawezesha kwa kuwapatia kiasi
cha shilingi laki sita (600,000) kwa ajili ya kujiendeleza.
Mbunge
wa Viti Maalumu (CCM) Iringa Rose Tweve akipokea risala ya wanawake wa
Kata ya Idunda wakati wa muendelezo wa ziara yake kata 107 ya
kuwahamisha wanawake wajiinue kiuchumi kwa kutumia vikundi pamoja na
kuwawezesha kwa kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa
ajili ya kujiendeleza.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM) akizungumza na
wananchi wa kata ya Maduma wakati wa muendelezo wa ziara yake kata 107
ya kuwahamisha wanawake wajiinue kiuchumi kwa kutumia vikundi pamoja na
kuwawezesha kwa kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwa
ajili ya kujiendeleza.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (CCM)akikabidhi kiasi cha
shilingi laki sita (600,000) kwa kikiundi cha wanawake wa Kata ya Maduma
kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya
kata 107 za Mkoa wa Iringa pia waliweza kupata kiasi cha laki moja
(100,000) kutoka kwa diwani wa kata hiyo.
No comments:
Post a Comment