Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka (katikati), akiongozana na Meneja wa mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, Mhandisi Simon
Jilima,(kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere, wakitembelea kukagua maendeleao ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, leo Juni 17, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la
Umeme Nchini, (TANESCO), limewahakikishia watanzania kuwa mradi wa umeme wa
gesi wa Kinyerezi II unaendelea kwa kasi kubwa na utakamilika kama
ilivyopangwa.
Hakikisho
hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka,
wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini
Dar es Salaam, ambao unatarajiwa kutoa Megawati 240 za umeme.
“Niwahakikishie
watanzania kuwa ifikapo Agosti mwakani (2018), mradi wa umeme Kinyerezi II
utakamilika na hivyo tutaongeza Megawati 240 kwenye gridi ya Taifa.” Alisema
Dkt. Mwinuka wakati akitoa majumuisho ya ziara yake.
Dkt.
Mwinuka alifuatana na wakurugenzi watendaji wasaidizi, Mhandisi Abdallah O.
Ikwasa, (anayeshughulikia Uzalishaji), Mhandisi Khalidi James,
(anayeshughulikia uwekezaji miradi) na Mhandisi Kahitwa Bishaija
(anayeshughulikia Usambazaji).
Dkt.
Mwinuka alisema watanzania wanahitaji umeme ulio wa uhakika na kwamba Serikali
kupitia TANESCO imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa
watanzania na hivyo kuchangia pato la taifa.
“Kama
mjuavyo serikali imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha Shirika linatekeleza
miradi hii na tayari shilingi Bilioni 110 zimetolewa na serikali katika
kutekeleza mradi huu wa Kinyerezi II.” Alifafanua Dkt. Mwinuka.
Awali
Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephens S.A.Manda, alisema, wataanza kuingiza
umeme kwenye gridi ya taifa kila mwezi kuanzia Desemba mwaka huu 2017 ambapo
Megawati 30 zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa.
“Tuna mashine
8 ambazo zitafua umeme huo kwa hiyo kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, tutaingiza
megawati 30 kwenye gridi ya taifa na tutafanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja
kwani tunaelewa kuwa serikali ambayo imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda,
tunaona umeme ni hitajio muhimu kwa hivyo kila tutakapokamilisha mtambo mmoja
tunaingiza umeme kwenye gridi ya taifa hatutasubiri kuwasha mitambo yote
minane.” Alisema Mhandisi Manda.
Mhandisi
Manda alisema, mradi mzima ambao umeanza kutekelezwa rasmi Machi 3, 2016,
utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 344,059,746.00 kati ya hizo asilimia 15
zimetolewa na serikali.
“ Kufikia
leo Juni 17, 2017, asilimia 63 ya ujenzi wa mitambo imekamilika, na tunahakika
ya kukamilisha ujenzi wa jumla kwa vile tayari mitambo yote inayohitajika
imeshalipiwa na mingine iko njiani inaletwa nchini.” Alifafanua na kuongeza
mitambo yote iliyoagizwa na TANESCO imo kwenye makontena 900 na tayari
makontena 400 na ushee yamekwishawasili na baadhi ya mitambo imefungwa na
tunatarajia mashine zingine kwenye hayo makontena yaliyosalia zitawasili nchini
wakati wowote. Alisema.
Akizungumzia
kuhusu makontena 20 yaliyokuwa yamezuiliwa na TRA bandarini, Mhandisi Manda
alisema, taarifa hizo hazina msingi wowote kwani kiasi hicho cha makontena 20
ni sehemu ya makontena 900 na tayari TANESCO imeshalipa fedha hizo za kodi na
mizigo hiyo imefika site.
Katika
ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Mwinuka ;pia alitembelea
mradi wa umeme wa upanuzi wa Kinyerezi II ambako nako ameridhishwa na kasi ya
ujenzi wake.
Mradi huo
ambao unasimamiwa na Mhandisi Simon Jilima, utawezesha ongezeko la megawati 35
na hivyo Kinyerezin I ambayo inatoa Megawati 150 itakuwa na uwezo wa kutoa
Megawati 185 za umeme.
Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda
Meneja wa mradi wa upanuzi Kinyerezi IMhandisi Simon Jilima
DKT. Mwinuka, (kulia), Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James, (katikati) na Meenja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen A.S.Manda, wakijadiliana jambo
Mitambo ikiteremshwa eneo la ujenzi
Mkurugenzi wa Business Times, Imma Mbuguni, (kulia) akizungumza jambo na Mhandisi, Khalid James
Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere(kulia), akiteta jambo na Kaimu Meneja Uhisano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme (Generation), Mhandisi Abdallah O.
Ikwasa(kulia), akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa Miradi wa TANESCO, Mhandisi Gregory Chegere
Mhariri Mtendaji wa Business Times, Bw. Imma Mbuguni, akizungumza ili kuoata ufafanuzi wa maswala kadhaa
Baadhi ya mitambo ikiwa eneo la ujenzi ikisubiri kuunganishwa
Mtandao wa nguzo za umeem ukiwa tayari kwa sehemu kubwa
Kaimu Meenja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji akifafanua baadhi ya mambo kuhusu namna Shirika hilo linavyotekeleza sera ya kusaidia jamii (Corporate Social Responsibility), ambapo alisema, licha ya shirika imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii sio tu kwenye maeneo ambako mradi unapita bali pia maeneo mengine na kutolea mfano wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera, kamati ya kikosi kazi cha kuokoa mazingira, na hata shule. Kushoto ni Dkt. Mwinuka na Mhandisi Khalid James
Dkt. Mwinuka akiwa amezungukwa na wasidizi wake akizungumza kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kinyerezi II
Dkt. Mwinuka (kulia), akiongozana na wakandarasi toka kampuni ya kijapani SUMITOMO amabao ndio wanajenga mradi huo
Dkt. Mwinuka (kushoto), Mhandisi Ikwasa(katikati) na Mhandisi Chegere
No comments:
Post a Comment