Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.
Joseph Nyamhanga (Wa pili kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Wizara
hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika
kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
Katibu
wa Baraza la Wafanyakazi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ramadhani Msafiri(Wa
pili kushoto), akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na
Wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha
Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
Mmoja
wa wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Ujenzi), Bw. Shukuru Sikunjema, akitoa maoni yake kwa Mwenyekiti Wa
Baraza la Wafanyakazi Eng. Joseph Nyamhanga katika kikao cha Baraza la
Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
Wafanyakazi
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi)
wakifuatilia maelekezo ya Baraza la Wafanyakazi wakati wa kikao hicho
kilichofanyika Mkoani Morogoro.
Wafanyakazi
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Wakiimba nyimbo ya ‘Solidarity forever’ kuonyesha mshikamano katika
utendaji kazi wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani
Morogoro.
Wafanyakazi
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga kikao cha Baraza la
Wafanyakazi kilichofanyika Mkoani Morogoro.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.Joseph
Nyamhanga, amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza majukumu yao kwa
weledi na uadilifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya
Tano.
Akisoma
hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Makame Mbarawa,
katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi leo, mkoani Morogoro, Eng. Nyamhanga,
ametoa wito kwa watumishi wote kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza
majukumu yao ili kuleta tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.
"Naliomba
baraza hili la wafanyakazi kuhakikisha linahamasisha watumishi wote wa Wizara
kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, weledi na ushirikiano ili
kuleta ufanisi", amesema Eng.Nyamhanga.
Aidha,
Eng. Nyamhanga amelisisitiza Baraza hilo kuandaa mkataba wa kupima utendaji
kazi wa watumishi katika majukumu yao ya kila siku ili kupima ufanisi wa
watumishi hao kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini.
Katibu
Mkuu Nyamhanga , amelitaka Baraza hilo kuweka mazingira maalum kwa
watumishi ikiwemo kuandaa mpango wa mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili
kuongeza ujuzi kwa watumishi wa Wizara hiyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la Ujenzi Bw. Samuel
Mticco, amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kutekeleza maagizo yote
yaliyosemwa katika Baraza hilo ikiwemo la uandaaji wa mkataba wa utendaji
kazi kwa watumishi.
Kikao
hicho cha siku moja cha Baraza la wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi pamoja na
mambo mengine kimekubaliana kupunguza matumizi ya fedha za Serikali yasiyo ya
lazima pamoja na kupambana na vitendo vya ufisadi na rushwa.
Imetolewa na kitengo cha
mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

إرسال تعليق