Wakuu
wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kupitia Jumuiya yake ya TSSA
(Tanzania Social Security Association), wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu
wa PSPF, Adam Mayingu (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
GEPF, Daud Msangi (wa pili kulia) wakiwa katika ziara ya kutembelea
kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga jana ambacho hakikuwahi
kufanya uzalishaji tangu kibinafisishwe. Ziara hiyo ya viongozi hao
ilikuwa ni kwa ajili ya kuona hali halisi ya kiwanda hicho ambacho kwa
sasa kipo chini ya mikono ya Serikali, Mifuko hiyo kwa pamoja kupitia
umoja wao wa TSSA wamedhamiria kuwekeza katika kwa pamoja katika sekta
ya ngozi, nyama na nguo.
Wakuu
wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kupitia Jumuiya yake ya TSSA
(Tanzania Social Security Association) wakipatiwa maelezo wakati
walipotembelea kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga, ambacho
hakikuwahi kufanya uzalishaji tangu kibinafisishwe.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi akisaini kitabu wakati walipotembelea
kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga, ambacho hakikuwahi kufanya
uzalishaji tangu kibinafisishwe. Kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya TSSA, Meshack Bandawe.
Wakikiangalia maeneo mbalimbali ya usindikaji Nyama.
Wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kupitia Jumuiya yake ya TSSA
(Tanzania Social Security Association) wakiendelea na ziara yao katika
kiwanda cha nyama kilichopo mjini Shinyanga.
Sehemu ya Majengo ya kiwanda hicho.

Post a Comment