Na Woinde Shizza,Arusha
Wanawake
wote hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kupima afya zao mara
kwa mara ili kuweza kujua matatizo ya mwili waliyonayo na kuyatatua
kabla ya madhara makubwa kutokea .
Hayo
yamebainishwa leo na mkurugenzi wa kampuni ya Phide entertaiment
Phidesia Mwakitalima wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
juu ya maandalizi ya wiki wanawake duniani ambayo inatarajia kuanza
March mbili ambapo kwa mkoa wa Arusha maadhimisho hayo yanatarajiwa
kufanyika kwa muda wa siku saba katika viwanja vya kumbukumbu ya
sheikh Amri Abeid .
Alisema
kuwa wanawake wengi wamekuwa awana tabia ya kupima afya zao mara kwa
mara kitu ambacho ni hatari mno kwani maisha ya sasa ukilinganisha na
hali ya tabia nchi ilivyo pamoja na vyakula ambavyo vinaliwa kwa kipindi
hichi.
Alisema
kuwa kutokana na tatizo hilo kuonekana hivyo kampuni ya Phide
entertaiment wameamua kuandaa kuandaa maadhimisho haya kwa kuwapa fursa
wanawake kujitokeza kupima afya zao bure ambapo alisema tukio zima
litafanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid kwa muda
wa siku saba ambapo alisema kuwa maadhimisho haya yataanza rasmi
March 2 hadi March nane.
" tamasha
hili kubwa linawapa fursa wanawake kuweza kupima Afya yako bure na
magonjwa ambayo yatapimwa katika wiki hii ni pamoja na Moyo, Kisukari,
Macho, na figo hivyo napenda kuwasihi wanawake wenzangu wote wajitokeze
kwa wingi waje wapime afya zao na wajijue vizuri "alisema Phide
Aidha
alisema kuwa mbali na kupima afya pia wiki hiyo itatumika kwa ajili ya
kuwapa wanawake ushauri juu ya kupima afya zao mara kwa mara ambapo
watawapa elimu ya kutosha .
"unajua
kipindi hichi wanawake wamekuwa wanapata magonjwa ya haina mbalimbali
na wingine wamekuwa wanapuuzia kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa
mara hivyo tamasha hili la wiki nzima litatumika kuwaelimisha wanawake
faida za kupima afya zao mara kwa mara"alisema Phide
Alimalizia
kwa kuwataka wanawake wote kutopuuzia wiki hiii kwani ni muhimu sana
kwa kujotokeza kupima afya zao na wajue mfumo mzima wa miiili yao ilivyo
pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya .


إرسال تعليق