
Waziri mwigulu nchemba akijadiliana jambo na mama mzazi wa chidi benz
Mh. Waziri ameyazungumza hayo kupitia ukurasa wake wa facebook, hii hapa kauli yake..
Nimekutana
na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo "Chid Benz"
ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya.Inasikitisha na
haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika
kwa pesa haramu.Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge,
wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika
awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa
namna yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa
dola.
Mbali ya
vyanzo vya taarifa tulivyonavyo,ni wajibu wa kila aliye RAIA MWEMA kutoa
taarifa zitakazo saidia kuangamiza biashara haramu ya madawa ya
kulevya.
Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada wanazozifanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida.
Unaweza kuimba,unaweza kufanikiwa,unaweza kutatua matatizo yako bila kutumia madawa ya kulevya.

Post a Comment