Ufuatao
ni muktasari wa thamani na faida ya kutuliza mawazo ya fikra kuleta
amani ya nafsi kupitia mafunzo ya” Meditation” ama kutafakari katika
jamii zetu.
Ulimwengu
wa leo wa karne ya 21 unakabiliwa na changa moto nyingi sana kimawazo
na maendeleo ya teknolojia kupitia sayansi na njia ya mitandao na
kuwawezesha wanaadam kuwa karibu sana ya mitandao kulikoni jinsi ya
karne zilizopita.
Uijio
huo wa maendeleo ya sayansi, pia umeleta mchanganyiko mkubwa kwenye
ubongo wa jamii ya kizazi cha leo na hata kile kilichopita pia, hasa
ukizingatia kwamba urahisi wa teknolojia na kuwa na uwezo wa habari na
matukio dunia kupitia mitandawazi na hatimae, pia kujenga mazingira
magumu kwa wale wasioitumia jinsi inavyostahili.
![]() |
Yoga Instructor Rumadha Fundi Katika mkao wa "Gomukhasana" zoezi la Yoga na kutafakari.
|
Dunia
ya kizazi kipya , kina kadiriwa na changa moto za kifra na mawazo,
tamaa, nia ya kuwa kama wenzao na taabu ya mawazo katika jamii yetu
inayoshawishiwa na hayo maendeleo tuliyonayo sasa. Mambo kama vile
“Stress” na shinikizo la kutaka kuwa na ushindani katika jamii
kumaendeleo ni moja ya vikwazo vikubwa vinavyo sababisha hata jamii
yetu iwe na msingi dhaifu kulinganisha na vizazi vya karne zilizopita,
japokuwa kuna mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia, lakini fikra
za wengi katika jamii hazina uvumilivu na amani ya mawazo mema katika
jamii zetu kutokana na vishawishi vya hayo maendeleo ya nayoletwa na
mitandawazi katika viganja vyetu kila sekunde.
Hivyo
basi, kutokana na muktasari huu, hapo ndipo haja ya kutuliza mawazo na
fikra za ubongo wa mwanaadam ni nguzo muhimu sana katika jamii zetu.
Hivyo umadhubuti wa fikra na akili ndio njia pekee inayoweza
kutoyumbishwa na vishawishi vinavyo shambulia akili ya mwanaadam
mitandaoni kwa nia isiyo elimisha, bali kuujaza ubongo na hali inayo
sababisha udhaifu wa mawazo, kutokuwa na utulivu itumiwapo kwa nia
isiyojenga na kuimarisha manufao ya akili na fikra.
Tafakari
“ meditation”, ndio chombo sahihi kupitia mafunzo ya sayansi ya Yoga na
mazoezi yake ili kuukabili mazingira na hali halisi ya maisha ya jamii
zetu.
Viumbe
tumeumbwa na tabaka au safu tano za ubongo zilizo kuwa na mfano wa
mauwa ya ndizi na kumenya safu moja hadi nyingine. Utegemea msingi wa
elimu ya fikra za mtu mwenyewe kuwa imara. Kila moja ya hizi safu au
tabaka zina thamani yake “Subtlety” na uchanga wake “Crudeness”
yategemea jinsi gani vikwazo vinavyo kabiri mawazo ya kila mtu binafsi.
Hii ndio mifano toka mwili, ubongo na fikra za mwanaadam na tabia
zake.
“Physical
Body” kwa lugha ya Sanskrit : Annamaya kos’a ikimaanisha mwili au
umbo la viumbe ambayo ni changa sana kimawazo na imeundwa kwa vigawanyo
vitano muhimu kimaisha. Kwa mujibu wa sanaa ya yoga, ujulikana kama “
Five fundamental factors”; yaani:
(a)Solid factor (b)Liquid factor (c)Luminous factor (d) Aerial factor (E)Ethereal factor.
1.”Conscious or Crude Mind” kwa lugha ya Sanskrit : Ka’mamaya
Ko’sa, hii ndio safu yenye kuingoza fahamu au ubongo wa mwanadau kwa
maisha ya kila siku na kawaida. Safu hii haina tofauti kimazingira na
viumbe wengine kimatendo, kama vile njaa, hamu ya kulala, kuwa na watoto
nk. haitofautiani na mnyama.
2.“Subconscoius
Or Subtle Mind” Kwa lugha ya Sanskrit: Manomaya Ko’sa. Hii ni safu
inayo tawala safu zote za chini yake na inawajibu au kazi nne muhimu,
yaani 1. Kumbukumbu, 2. Kuwaza, 3. Kusikia uchungu na furaha, na 4.
Ndoto. Hizo ndio kazi za hii safu ya ubongo wa mwanadaam. Mifano ya watu
wenye hizi sifa ni kama vile; Albert Einstein aleye buni “Theory of
Relativity”, Vasily Mendeleev aliyebuni “Periodic Table”, Charles
Darwin aliyebuni “Theory of Evolution & Origin of Species”,
Michaelangelo, aliye andika “A seizure of the Soul” na William Blake
aliye kuwa “ Visionary Poet and Artist”. Wote wale walioweza penya upeo
wao wa fikra katika safu za ubongo wao huendeleza uwezo wa hali ya juu
sana kimawazo kutokana na utulivu wa mawimbi ya fikra zao zinazo watenga
na watu wakawaida.
3. “Supramental Mind” Kwa lugha ya Sanskrit : Atima’nasa Ko’sa. Yaani “Akili ya kiwango cha juu sana”.
Hii ni safu au tabaka la ubongo ambapo ubunifu , sanaa na ujuzi wa fikra”Intuition” hutendeka katika safu hii.
4. “Subliminal Mind” Kwa lugha ya Sanskrit: Vijina’namaya Ko’sa.
Hii
ni safu au tabaka la ubongo linalo tawala aina pekee za vipaji. Moja ya
vipaji vyake ni kuwa siwa kawaida, utabiri kujuwa ishara ya matokea
yajayo na yaliyopo.
Hivyo
basi, bila ya kuchambua kwa kina kirefu moja ya tabaka hizi kwa
muktasari tu, njia pekee kuu ya kuiongoza akili ya mwanaadam au mawazo
ya mtu, ni kupitia utulivu wa mawimbi ya ubongo kwa njia ya kutafakari
na mazoezi ya sanaa ya Yoga. Katika safu hii, subira, utulivu wa mawazo,
furaha na maendeleo ya kiroho chimbuko lake lipo hapa.
5. “Subtle Causal Mind” Kwa lugha ya Sanskrit: Hiran’yamaya Ko’sa.
Hii
ujulikana kama safu au tabaka la dhahabu ”Golden layer”, kutokana na
ubora wa kina chake katika ubongo wa mwanadaam. Ni safu mahili yenye
kunga’ra na watakatifu wa dini nyingi ni mfano wa ubora wa fikra zao
kuwa upeo wa mawazo yao unalingana la safu hii. Miujiza mingi pia utokea
mwanaadam anayepenya katika safu kimawazo.
Mazoezi
ya sanaa ya Yoga yanaimarisha mawazo na nguvu za mwili kupitia mbinu
zake za mafunzo yenye mwigo wa mikao mingi ya wanyama. Ubongo wa
mwanaadam unatoa mawimbi au “Waves,” “Beta waves” (13 kwa sekunde),
Alpha waves”(8 kwa sekunde), Theta waves”(4 kwa sekunde), na “Delta
wave” (1 kwa sekunde) mengi na kila safu ina namba ya mawimbi yake na
hatimae kufikia uwezo wa kuwa tulivu na kuwa na hizo sifa zilizotajwa
hapo juu.
Haya
maelezo yamenukuliwa na mkufunzi wa sanaa hiyo ya Yoga, Rumadha Fundi
toka katika jarada la mafunzo ya Yoga “Ananda Sutram” toka kwenye
maktaba ya chuo alicho soma na kuhitimu sanaa hiyo 1987. “ College of
Neo- Humanist Studies”, Ydrefors, Gullringen, Sweden na Culcutta, West
Bengal, India.


Post a Comment