Polisi katika
jimbo la Marekani la Mississippi wanasema wanachunguza uhalifu wa chuki
baada ya Kanisa linalotumiwa na watu weusi kuteketezwa na kisha kuchorwa
maneno ya kusema: "Mpigie kura Trump".
Kanisa hilo linalopatikana eneo la Greenville lilijengwa miaka 111 iliyopita.
Msimamizi wa kituo cha zima Moto alisema kuwa moto katika Kanisa la Hopewell Missionary Baptist Church uliwashwa makusudi.
Shambulio hilo limetokea wiki moja kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika Jumanne wiki ijayo.
Maafisa wanasema ujumbe ulioandikwa kwenye jumba hilo ni wa kuzua hofu.
Meya wa
Greenville, Mississippi amesema kisa hitendo hicho ni cha "chuki na
woga" na s"shambulio la moja kwa moja dhidi ya uhuru wa watu kuabudu".
Kisa hicho
kinawakumbusha watu kuhusu visa vya kuchomwa moto kwa makanisa ya watu
weusi miaka ya 1950 na 1960, watu weusi waliokuwa wanapigania haki zao.
Maafisa wa FBI wakishirikiana na wachunguzi wa jinai wa jimbo la Mississippi kwa sasa wanaendelea na uchunguzi.


Post a Comment