Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefakiwa kukamata watu
watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi hatari ambao wamekuwa wakishiriki
matukio mbalimbali ya uhalifu kwa kutumia silaha.
Watu
hao wanaodaiwa kuwa majambazi walipatikana na bunduki 23 za aina
tofauti tofauti, Risasi 835, kifaa cha kuzuia risasi kuingia mwilini
tatu (Burret Proof), Sare za Polisi, Pingu 48 pamoja na Radio 12 za
mawasiliano.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika viwanja vya kanda maalum, Kamanda wa
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema
kuwa majambazi hao walikuwa na mtandao mkubwa ikiwa ni kununua silaha
nje ya nchi kwa ajili ya kufanyia uhalifu katika maeneo mbalimbali.
Kamanda
Sirro amesema baada ya tukio hilo timu ya polisi ya upelelezi iliweka
mtego na kufanikiwa kukamata majambazi watatu maeneo ya Mbagala, Keko na
Kawe.
Kamanda
Sirro amesema katika mahojiano walikiri kufanya tukio katika benki ya
Habib African maeneo ya Kariakoo 2014 na Stanbic 2014.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
akionyesha kifaa cha kuangalia wakati wakifanya uhalifu majambazi kwa
waandishishi wa habari ikiwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikitumika
na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo
jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
akionyesha bunduki kwa waandishi wa habari ikiwa ni sehemu yabunduki
zilivyokuwa zikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya
kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment