Pages

September 1, 2016

DC KASULU AFUNGA MAFUNZO YA OPERESHENI MAGUFULI (JKT) KAMBI YA 825 KJ KIGOMA

Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akikagua paredi ya vijana 1140 wa operesheni Magufuli kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha 825 KJ kilichopo Mtabila katika Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma.

Na Abel Daud, Globu ya Jamii, Kigoma

Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya operesheni Magufuli (kwa mujibu wa sheria) kutoka wilayani hapo kwenda kutekeleza falsafa ya hapa kazi tu.

Hayo ameyasema alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana 1140 operesheni Magufuli kwa mujibu wa sheria katika kikosi cha 825 KJ kilichopo Mtabila katika Wilaya ya Kasulu na kuwataka kwenda kuungana na watanzania wengine wote katika kuiamini kuitekeleza na kuiishi falsafa ya hapa kazi tu kwa vitendo.

Akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi, Mkuu wa kambi ya 825 KJ, Meja George Kazaula amesema kikosi kimefanikiwa kutengeneza madawati 1074 ikiwa ni agizo la Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli.

Pia ameelezea changamoto zinazoikabili kambi hiyo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa umeme wa gridi ya taifa pamoja na miundombinu ya barabara kuwa mibovu hali inayopelekea matumizi makubwa ya uendeshaji wa umeme wa genereta pamoja na matengenezo ya mara kwa mara ya magari ya kikosi.

Nae mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga taifa hapa nchini Luten col. Philipo Mahende amewataka vijana hao kuwa wazalendo wa kweli ambao watakuwa tayari kulilinda taifa kwa gharama yoyote ile ili amani,umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania unakuwa endelevu, na kuwaomba kujiepusha na kutokuwa miongoni mwa watanzania wachache wanaoshabikia mgawanyiko miongoni mwetu kwa misingi ya itikadi za kisiasa,kidini au mahali anapotoka mtu.

Akisoma lisara kwa mgeni rasmi mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo ameiomba serikali kuiongeza bajeti Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa ili vijana wengi wapate nafasi kujiunga na mafunzo ya JKT ili waweze kujifunza uzalendo na shughuli za uzalishaji mali ili kuwatengenezea uwezo wa kujiajiri wenyewe pasipo kuitegemea Serikali.
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akitoa zawadi kwa baadhi ya vijana waliofanya vizuri katika mafunzo hayo
Vijana hao Wakipita kwa mwendo wa haraka.
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akipokea heshema ya kijeshi kutoka kwa vijana wanaohitimu
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi wa kwanza kushoto akielekea yalipo madawati.
Baadhi ya madawati yaliyotegenezwa.
Baadhi ya vijana wa JKT Mtabila wakiendelea na kazi ya kupaka rangi madawati.
Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akiangalia madawati yaliyotegenezwa kambini hapo.
Vijana wanaomaliza mafunzo ya opeteshen Magufuli wakipita kwa mwendo wa kasi mbele ya mgeni rasmi.
Meja George Kazaula akisoma taarifa fupi


Mkuu wa Wilaya ya kasulu Kanali Martin Mkisi akitoa hotuba

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...