Pages

September 24, 2016

Airtel yaipongeza Kilimanjaro Queens

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imeipongeza Timu ya wanawake Tanzania ya Kilimanjaro Queens kufatia ushindi wa walioupata katika michuano ya Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 maarufu kama CECAFA 
 Timu ya kili Queen iliyosheheni vijana kutoka Airtel Rising Stars imeibuka washindi wa michuano hiyo baada ya kuichapa harambee Queens ya Kenya bao 2-1 akiongea wakati wa timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel leo , Mwenyekiti wa soka la wanawake Tanzania , Bi Amina Karuma alisema" Tumekuja hapa Airtel leo na kuleta kombe hili kwani tunathamini sana mchango mkubwa unaofanywa na Airtel kupitia program ya Airtel Rising Stars ambayo imetuwezesha kupata wachezaji mahiri na waliotuwezesha kuleta ubingwa huu nchini. 
"Tunajisikia faraja kuona Airtel iko bega kwa bega na sisi katika kuhakikisha soka la wanawake linaendelezwa na kukua kwa kasi, juhudi hizi zilizofanywa kwa miaka sita sasa zimezaa matunda kwa timu ya wanaume ya Serengeti boys na sasa kwa timu yetu ya Kilimanjaro Queens. 
"Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza na kuwaomba waendelee kushirikiana nasi katika kukuza, kulea na kubaini vipaji chini ya mpango wa Airtel Rising Stars ambao umekuwa tija skwa maendeleo ya soka nchini", alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso aliwapongeza wachezaji wa Kili Queens kwa ushinid wa kishindo kikubwa na kuahidi kuendelea kudhamini michuano ya Airtel Rising Stars ili kubaini vipaji vipya zaidi na kuwawezesha vijana kuzifikia ndoto zao ili kutimiza dhamira ya kampuni yake chini ya Mpango wake kabambe wa Airtel FURSA.
Kufatia ushindi huo Airtel imewazawadia wachezaji hao kila mmoja kiatu cha mpira ikiwa ni motisha kwa wachezaji kuchezea na kuendelea kufanya vizuri na kupata vifaa bora vya michezo wachezaji wa 
Kili Queens wanane walitoka katika michuano ya Airtel Rising Stars ambao ni pamoja na Stumai Abdallah, Sherida Boniface, Anna Ezron , Anastazia Antony, Amina Ally, Donisia Daniel, Najiat Abbasi na Maimuna Khamis




 Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akiwapokea wachezaji  wa Kili Queens  wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel makao makuu
 wachezaji wa Kili Queens wakiingia katika ofisi za Airtel  wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel na kushukuru kwa mchango wa Airtel katika kuinua vipaji vya vijana kupitia program ya Airtel Rising Stars
 wachezaji wa Kili Queens wakiingia katika ofisi za Airtel  wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel na kushukuru kwa mchango wa Airtel katika kuinua vipaji vya vijana kupitia program ya Airtel Rising Stars
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (katikati), akimpongeza Nahodha wa timu ya mabingwa wa Kombe la Challenge la Afrika Mashariki na Kati 2016, Kilimanjaro Queens, Sophia Mwasikili wakati timu hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Asilimia kubwa ya wachezaji wa Kili Queens ni matunda ya mashindano ya Airtel Rising Star. Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto), akimpongeza Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi wakati timu ya mabingwa wa Kombe la Challenge la Afrika Mashariki na Kati 2016, Kilimanjaro Queens, ilipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma na (wa pili kulia), ni Nahodha wa timu hiyo,  Sophia Mwasikili.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (katikati),Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi (kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda (kushoto) na nahodha wa timu ya Kilimanjaro QueensSophia Mwasikili wakilishikilia kombe la mabingwa wa Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 lililotwaliwa na Kili Queens, wakati timu hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  na nahodha wa timu ya Kilimanjaro QueensSophia Mwasikili wakilishikilia kombe la mabingwa wa Challenge Afrika Mashariki na Kati 2016 lililotwaliwa na Kili Queens, wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel
 Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akiongea na timu ya Kilimanjaro Queens na waandishi wa habari  wakati  timu  hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni ya Airtel  jijini Dar es Salaam . Asilimia kubwa ya wachezaji wa Kili Queens ni matunda ya mashindano ya Airtel Rising Star.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso  akiongea na timu ya Kilimanjaro Queens na waandishi wa habari  wakati  timu  hiyo ilipotembelea makao makuu ya kampuni ya Airtel  jijini Dar es Salaam. wakishuhudia ni  Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Kandanda nchini, Salum Madadi (katikati) akifatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda
 wachezaji 8 wa Kilimanjaro Queens ambao ni matunda ya Airtel Rising Stars wakiwa katika picha ya pamoja wakati timu  hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel.  wachezaji hawa waliibuliwa kutoka katika michuano ya Airtel Rising Stars iliyopita
 Afisa uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (aliyeshikilia kombe) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji 8 wa Kilimanjaro Queens ambao ni matunda ya Airtel Rising Stars pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel Tanzania. 
Timu ya wanawake Tanzania ya Kilimanjaro Queens ikiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Airtel na TFF wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...