Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kitengo kinachoshughulikia Tsunami, Ardito Kodijat
akifungua mafunzo hayo kwa kuwaeleza washiriki aina ya mafunzo ambayo
watapatiwa
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues akitoa neno
la ufunguzi kwa niaba ya UNESCO Tanzania na kueleza sababu ya kufanyika
mafunzo hayo.
Mkuu
wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hewa nchini
(TMA, Dk. Ladislauds Chang`a akizungumza jinsi TMA imejipanga kuendeleza
kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Tsunami na kuwataka Watanzania kuwa na
utaratibu wa kufatilia hali ya hewa nchini hasa katika kipindi hiki
ambacho ni kuna mabadiliko ya tabia ya nchi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard
Chamuriho akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo yanayohusu kuwapa elimu
washiriki ya kuhusu Tsunami.
Baadhi ya washiriki ambao wameshiriki katika mafunzo hayo ambayo yanataraji kufanyika kwa siku tano.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
Kutokana
na kuwa na athari kubwa ambazo zimekuwa zikisababisha majanga makubwa,
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) limeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatashirikisha
watu mbalimbali nchini ili kuwapa elimu kuhusiana na majanga.
Akizungumzia
Mafunzo hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira
Rodrigues alisema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kupata
elimu kuhusiana na Tsunami ikiwa ni pamoja na madhara ambayo
yanasababishwa na hivyo ni matarajio yao watakuwa mawakala wazuri kwa
kusambaza elimu hiyo kwa Watanzania wengine.
“Watu
wengi wamepoteza maisha tukumbuke Tsunami la Japan zaidi ya watu 20,000
walipoteza maisha kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni
kwa kiasi gani Tsunami linakuwa na madhara hata kama limetokea mbali na
hapa,” alisema Bi. Rodrigues.
Nae
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard
Chamuriho alisema ni vyema kwa watanzania kupata elimu hiyo kutokana na
madhara ambayo yamekuwa yakitokea ikiwemo Tsunami la mwaka 2004 ambalo
lilitokea eneo lililombali na bahari ya Hindi lakini lilisababisha
athari nchini na kusababisha vifo vya waogeleaji watano.
“Mafunzo
haya yanatakiwa kufanyika kwa wananchi wote na mwezi Septemba
yatafanyika mengine na yatahusisha watu wengi lengo kila Mtanzania ajue
nini cha kufanya siku athari zikitokea wajue nini wanafanya ni muhimu
kwa kila mtu kujua athari za Tsunami hata likitokea mbali,” alisema Dk.
Chamuriho.

Post a Comment