MFUKO
wa kichocheo wa SAGCOT wasaini makubaliano ya utekelezaji wa Mradi na
kampuni zilizoomba ufadhali wa Fedha kwaajili ya uimarishaji wa Viwanda
pamoja na ukuzaji wa Kilimo hapa nchini jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe akizungumza katika
hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo amesema kuwa Mfuko wa SAGCOT
wamesaini mikataba kwaajili ya kibiashara kwanzia mtaji kati ya Dola Za
Kimarekani milioni 50 hadi 100 zitakuwa zikitolewa kwa miradi kupitia
madirisha ya Matching Grant Fund(MGF) ambao utakuwa ukitatua changamoto
za wakulima na masoko yao.
Pia
amesema kuwa dirisha jingine ni la Social Venture Capital(SVC) dirisha
hili litalenga kuwzesha kujengwa kwa viwanda vikubwa ba vya kati ili
kutoa masoko kwa wakulima hasa wa maeneo amayo yana mazao mengi lakini
hakuna kiu ya sekta binafsi ya kuwekeza katika maeneo hayo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe akizungumza na
wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo
hapa nchini jijini Dar es Salaam leo wakati
wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa
Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye
kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko.
Katibu Mkuu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, John Kyaruzi akizungumza na wawakilishi
wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo hapa nchini
jijini Dar es Salaam leo pamoja na kuwakaribisha wawakilishi wa
wakulima kwenda kuelezea kazi zao mbele ya Mgeni rasmi kutoka wizara ya
Viwanda, Biashara na uwekezaji.
Mwenyekiti
kampuni ya Cane Care Limited, Dr. George Mlingwa akifafanua jambo mbele
ya Mgeni Rasmi na mwakilizshi wa Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Joel
Malongo kuhusiana na kampuni yake ya Kilimo cha Miwa pamoja na hatua
za uandaaji wa utengenezaji wa Sukari hapa nchini katika kiwanda chake
Kidogo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo akizungumza na vongozi wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, wawakilishi
wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo jijini Dar
es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa
Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka
kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo (Mwenye tai nyekundu waliosimama) akisuhudia wawakilishi wa vyama vya wakulima wakisaini
mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo
wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro
cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo katikati kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe na Katibu Mkuu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, John Kyaruzi wakiwa katika mkutano huo wa wakati
wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa
Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye
kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko jijini Dar es
Salaam leo.


Baadhi
ya wadau wakiwa katika mkutano wa kusaini mikataba ya makubaliano ya
ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni
zilizoibuka kidedea kwenye kinyang'anyiro cha kuomba ufadhili kutoka
kwenye mfuko jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.












Post a Comment