Pages

June 26, 2016

RAIS DK. MAGUFULI AFUTURISHA MAKUNDI MBALIMBALI YA VIONGOZI, WALEMAVU WA NGOZI, WASIOJIWEZA PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir wakati wakielekea kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa  Salum.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir mara baada ya kufuturu na makundi ya watu mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir , Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum pamoja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakiwa wamesimama wakati wa dua mara baada ya kufuturu.

Baadhi ya wananchi wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mtoto mwenye ulemavu wa ngozi aliyetambulika kwa jina moja la Yusuph mara baada ya kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya makundi ya akina mama waliojumuika katika futari hiyo. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...