SERIKALI
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitiliana saini mkataba wa kufungua
Ofisi ya Konseli ya Heshima jijini Toronto, Canada. Mkataba huo ulitiwa
saini kati ya Konseli wa Heshima, Bw. Deepak Ruparell na Mhe. Jack
Mugendi Zoka Balozi wa Tanzania Nchini Canada ambaye aliiwakilisha
Serikali ya Tanzania. Tukio hilo lilifanyika kwenye ofisi za Ubalozi wa
Tanzania zilizopo jijini Ottawa nchini Canada.
Mhe. Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Canada (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell (kushoto) na Bw. Adtya Jha (kulia), Mjumbe wa National Capital Commission, Ottawa ambaye alifuatana na Konseli wa Heshima Mteule.
Mhe.
Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Canada (mwenye tai ya Bendera ya Taifa) akiwa katika picha ya pamoja na
Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak Ruparell (kulia kwa Balozi),
akifuatiwa na Bw. Richard Masalu, Afisa wa Ubalozi na mwisho, kushoto
ni Bw. Leonce Bilauri, Mkuu wa Utawala Ubalozini. Kushoto kwa Mhe.
Balozi ni Bibi Aziza Bukuku akifuatiwa na Bw. Paul Makelele ambao ni
maafisa wa Ubalozi.
Tukio
la kutiliana saini mkataba wa kufungua Ofisi ya Konseli ya Heshima
jijini Toronto, Canada likifanyika kati ya Mhe. Jack Mugendi Zoka,
Balozi wa Tanzania nchini Canada ambaye anaiwakilisha Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Konseli wa Heshima Mteule, Bw.
Deepak Ruparell , likishuhudiwa na maafisa wa Ubalozi.
Baada
ya tukio la kutiliana saini mkataba, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi Zoka na Konseli wa Heshima wa
Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak Ruparell , wanaonekana
wakibadilishana nyaraka za tukio hilo.
Mhe.
Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Canada akimkabidhi Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw.
Deepak Ruparell picha ya Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere
kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Mhe.
Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Canada akimpa maelezo Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto,
Bw. Deepak Ruparell na hatimaye kumkabidhi Nembo na Bendera ya Taifa
kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
Mhe.
Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Canada akimkabidhi Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw.
Deepak Ruparell nakala ya Mkataba wa Vienna wa mwaka 1963 kuhusu
Utendaji wa Shughuli za Kidiplomasia na Taratibu za Kikonseli ikiwa
ni moja ya vitendea kazi muhimu kwa matumizi ya ofisi.
Mhe.
Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Canada (mwenye tai ya Bendera ya Taifa) akiwa katika picha ya pamoja na
Konseli wa Heshima wa Tanzania, jijini Toronto, Bw. Deepak
Ruparell (kulia kwa Balozi) pamoja na wafanyakazi wote wa Ubalozi mara
baada ya kuhitimisha tukio la kutiliamna saini mkataba.
Mhe.
Jack Mugendi Zoka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini
Canada akimkaribisha Konseli wa Heshima Mteule, Bw. Deepak
Ruparell kwenye chumba cha wageni cha Ubalozi mara baada ya kuwasili.
Post a Comment