Pages

May 30, 2016

KITUO CHA MIKUTANO CHA AICC CHAKABIDHI MADAWATI 100


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda (kushoto) akipokea madawati kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa Itifaki na Uhusiano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Catherine Kilinda. AICC imechangia madawati 100 kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha shule zinakuwa na madati ya kutosha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kupokea msaada wa madawati 100 kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Katikati ni Afisa Mwandamizi wa Itifaki na Uhusianoi wa AICC, Catherine Kilinda.
Kituo cha Mikutano cha KimataifaArusha (AICC)kimemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Ntibenda madawati 100 yenye thamani shilingi milioni nane ili kupunguza tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa huo.

Akipokea madawati hayo jijini Arusha jana, Ntibenda amesema kwamba msaada huo ni sehemu ya  juhudi za serikali mkoani Arusha kuwashirikisha wadau wa  maendeleo ili kuhakikisha shule zote za mkoa huo zinakuwa na madawati ya kutosha.

“Napenda niishukuru sana  AICC kupitia kwa  Mkurugenzi  Mwendeshaji  Elishilia Kaaya  kwa  kuitikia vema wito wa serikali ya mkoa wa kuomba wadau wasaidie  kuondoa tatizo la upungufu wa madawati katika mkoa wetu”, alisema Mkuu wa Mkoa.

Alitoa  wito   kwa wadau  mbalimbali mkoani Arusha wakiwemo wafanyakazi wa ofisi ya  Mkoa wa Arusha nao  kujitokeza ili kuunga mkono juhudi         za serikali za   kuhakikisha kila  mwanafunzi ana kaa katika dawati.

Akizungumza baada ya kukabidhi madawati hayo, Afisa Mwandamizi waItifakina Uhusiano  wa AICC, Catherine Kilinda amesema kwamba AICC kama shirika la  umma linawajibu  wakuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.

“Sisi kama shirika la umma linalojiendesha kibiashara  tunaona fahari kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia  wa kuhakikisha watoto wetu wa shule  hawakai chini na ndio maana  leo hii  tumekabidhi msaada huu ikiwa ni kuunga mkono juhudi za  Mheshimiwa Rais katika kuinua sekta ya elimu”, alieleza Catherine.

AICC ambayo inajihusisha na kutoa huduma za Mikutano, upangishaji w ofisi na nyumba pamoja na kutoa huduma za afya, imekuwa ikitumia sehemu ya faida katika kusaidia jamii hasa katika sekta ya elimu.



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...