Picha
Wanawake Kutoka Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha Pamoja na Viongozi na
Wakufunzi Kutoka Tasisis ya Manjano Foundation Wanaoudhuria Mafunzo ya
Ujasiriamali Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation.
Awamu
ya Sita ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa Mkoa wa Arusha yameanza leo.
Wanawake 30 wa jiji la Arusha Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali
kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na
mtaalamu wa mambo ya Biashara Bw Alphonce Masagga na mama Shekha Nasser.
Mafunzo haya yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa Kitanzania
kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri
ndani ya Tasnia ya urembo. Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Golden Rose Hotel, Jijini Arusha.
Mafunzo
haya yamegawanywa katika Sehemu mbili ili kumsaidia mjasiriamali wa
kike kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara
namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio
wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali fedha na muda na pia
namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake.
Awamu
ya pili mshiriki anafundishwa matumizi sahihi ya vipodozi kuendana na
wakati, mfano office makeup, day makeup, evening na namna ya kumpamba bi
harusi. Pia wanafundishwa namna bora ya kutumia vipodozi vya LuvTouch
Manjano kwa lengo ya kuwa kila mshiriki atakayehitimu mafunzo haya aweze
kujiajiri na kujitegemea kwa kuendesha maisha yake ya kila siku kwa
kuwapambamba watu wenye shuguli mbalimbali.
Pamoja
na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwa na mwanamke mmoja mwenye
mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa lengo la
kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima.
Baada
ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation
inatoa mikopo kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini
ya uangalizi maalum wa taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila
mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea

إرسال تعليق