Mkuu wa Shule amewapongeza sana Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2015 na kwa Ufaulu mzuri. Pia amewamwagia sifa kemkem Walimu kwa ujumla huku akipongeza Wazazi, uongozi wa shule hiyo kwa kufanikisha siku hii kwa kumshukuru Mungu kwani amejibu Sala zao na kuwawezesha wote kufaulu vizuri mtihani wao wa Taifa. Mwaka 2015 Wanafunzi 47 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Taifa kidato cha Nne, Wanafunzi 36 wamefaulu kwa Daraja la kwanza na Wanafunzi 11 wamefaulu kwa daraja la pili. Katika matokeo haya Shule imekuwa ya 2 kati ya shule 192 Kimkoa na ya 17 kati ya Shule 3452 Kitaifa. Aidha , wanampongeza Mkuu wa Shule, Mkurugenzi na Uongozi mzima kwa uwezeshaji mkubwa sana hadi kufikia mafanikio hayo.
إرسال تعليق