Dar es Salaam, Februari 17, 2016 - Fastjet imepunguza mtiririko wa safari zake kwenye njia ya Kilimanjaro Tanzania na Nairobi Kenya kuanzia Jumatatu Februari 15, 2016.
Fastjet
ambao awali walikuwa wanatoa safari za kila siku kwenye njia hii hivi
sasa watakuwa wanafanya safari kutoka Uwanja Ndege wa Kimataifa wa
Jomo Kenyatta hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mara
mbili kwa wiki siku za Ijumaa na Jumapili tu.
Mabadiliko
ya mtiririko wa safari utazifanya ndege za fastjet kuondoka Nairobi
kila Ijumaa na Jumapili saa 5.40 na kutua Kilimanajaro saa 6.40 na
safari ya kurudi ndege itaondoka Kilimanjaro saa 7.10 na kutua Nairobi
saa 8.10.
Kupunguzwa
kwa safari hizo kumetokana na kuwepo kwa mahitaji kidogo miongoni mwa
wateja nyakati za wiki kutoka masoko yote mawili ya Kilimanjaro na
Nairobi na hivyo kufanya safari za ndege za kila siku kutokuwa nzuri
kibiashara kwenye siku hizo.
Shirika
hilo limesema kuwa lengo lake ni kurejesha safari hizo kwenye njia ya
Kilimanjaro –Nairobi pindi tu wateja wake watakapohitaji.
Safari za kila siku za kutoka Dar es Salaam na Kilimanjaro hadi Nairobi zilianza Januari 11, 2016.
Mahitaji
ya abiria kwa safari za ndege kwenye njia kubwa ya kibiashara kati ya
majiji ya Dar es Salaam na Nairobi ambayo kwa pamoja yana idadi ya
watu zaidi ya milioni nane yamekuwa ni ya kuridhisha na fastjet iko
kwenye mawazo kuwa ndege moja ni lazima iongezeke kwenye safari kati ya
majiji haya miwili katika siku za usoni.
Matokeo
ya safari za fastjet kwenda Nairobi kutoka Dar es Salaam yamekuwa ni
makubwa ambako kunaelezwa na ukweli kuwa nauli zinazotolewa na mashirika
ya ushindani kati ya nchi hizo mbili zimeshuka kwa kiwango cha hadi
asilimia 40 tangu fastjet waanze safari zake.
Nauli
za fastjet kwa kiwango kikubwa zipo chini kuliko zile zinazotozwa na
mashirika mengine kwa safari za moja kwa moja kati ya Nairobi/Dar es
Salaam ambapo nauli zinaanzia dola 80 kwa safari moja.
Nauli
hizo hazijumuishi kodi ya serikali ambayo ni dola 49 kuondokea Tanzania
na dola 40 kuondokea Kenya na hivyo fastjet kupendekeza wateja wake
kufanya maandalizi mapema ili kutumia fursa hiyo ya tozo la nauli nafuu.
Hata
hivyo fastjet inasisitiza kuwa kupunguza safari kwenye njia kati ya
Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa ya kuongeza uwezo kwenye njia za
kikanda zilizopo na hali kadhalika uwezekano wa kuzindua njia nyingine
mpya ya kikanda katika siku za karibuni.


إرسال تعليق