KIFO CHA LETICIA NYERERE.

Aliyekuwa mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Marehemu Leticia Nyerere. 

Dar es Salaam.
 Aliyekuwa mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Leticia Nyerere amefariki dunia Maryland nchini Marekani alikokuwa akipatiwa matibabu. 

Leticia kabla ya mauti kumkuta, alijiunga na CCM mwaka jana baada ya kutofautiana na viongozi wa chama hicho cha upinzani. 

Kutokana na kifo hicho, Rais John Magufuli jana alikwenda nyumbani kwa mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam kumpa pole ya msiba huo wa mkwewe. 


Pia, aliwapa pole wanafamilia na kuwaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba. 
Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alimuambia Rais Magufuli kuwa familia hiyo inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka Marekani na baadaye itatoa taarifa. 

Akizungumzia msiba huo, Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda alisema walitarajia kukutana na wanafamilia kuzungumzia kifo hicho. 


“Ukweli hadi sasa hakuna mtu anayejua kinachoendelea baada ya kifo hiki. 

Ndiyo kila utakayemuuliza hawezi kukuambia chochote kwa sababu tukio hili lilitokea usiku,” alisema Shibuda.MWANANCHI

Post a Comment

أحدث أقدم