|
Mmoja
wa Wakurugenzi wa Mtandao wa Asasi za Kiraia za Uangalizi wa Chaguzi
(TACCEO), Hebron Mwakagenda (katikati), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Makao Makuu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Dar es Salaam leo mchana, kuhusu Polisi kudaiwa kufanya uvamizi na
kuwakamata waangalizi, vifaa binafsi na vifaa vya Kituo cha Uangalizi wa
Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC), Mbezi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa LHRC,
Imelda Urrio na Kaimu Mkurugenzi wa Utetezi wa LHRC, Anna Henga |
Kaimu
Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio (wa tatu kutoka kushoto), akisisitiza
jambo katika mkutano huo. Kutoka kulia na Mwanasheria wa LHRC, Halord
Sungusia, Mwakilishi wa Taasisi ya YPC, Maria Kayombo na Mwakiliashi wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Melikizedeck Karol.
|
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
TACCEO yalaani kukamatwa waangalizi wa uchaguzi
Na Dotto Mwaibale
ASASI
za Kiraia za Uangalizi wa Uchaguzi (TACCEO), pamoja na Kituo cha Haki
za Binadamu (LHRC), wamelaani kitendo cha kuvamiwa na Jeshi la Polisi,
Oktoba 29, mwaka huu na lile la kukamata vitendea kazi na waangalizi wa
uchaguzi 36.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo mchana, Kaimu Mwenyekiti wa TACCEO, Hebron
Mwakagenda, alisema Jeshi la Polisi lilivamia kituo cha LHRC, kilichopo
Mbezi na kudai kuwa, waliagizwa na mamlaka husika kuwakamata waangalizi
na vifaa vya kieletroniki vilivyokuwa vikitumika katika mchakato huo.
Mwakagenda
alisema polisi hao waliongozwa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya kipolisi
Kawe, ASP Mgonja, ambapo maofisa wa uangalizi walieleza kuwa, walipata
taarifa kituo hicho kinakusanya na kunasambaza taarifa za matokeo
zisizo rasmi.
"Katika
mchakato huo, polisi walikusanya vifaa vyetu na kukamata kompyuta za
mezani 24, mpakato tatu na simu za mkononi za waangalizi 25," alisema
Mwakagenda.
Alisema
baada ya tukio hilo, vifaa hivyo vilichukuliwa na kukabidhiwa kituo cha
kati na baadaye kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi huku, baadhi
ya waangalizi wakichukuliwa kwa ajili ya kutoa maelezo na baadaye kupata
dhamani.
Watu hao wametakiwa kurudi kituoni hapo Oktoba 30, mwaka huu kwa ajili ya kumalizia maelezo yao.
"Mchakato
huo la kurudi Oktoba 30, mwaka huu lilifanikiwa na kwa sasa waliambiwa
warudi leo, kwa taratibu nyingine za kipolisi," alisema Mwakagenda.
Mwakagenda
alisema uvamizi huo uliofanywa na jeshi la polisi ni wa kudhoofisha
ustawi wa demokrasia nchini kwani, wasababisha kuwatishia wananchi
kushiriki katika mambo yanayohusu mchakato wa chaguzi nchini.
"Katika
hili ni kama wameondoa dhana nzima ya ushiriki kikamilifu wa sekta ya
umma na binafsi katika kutoa maoni ya kuboresha demokrasia na
uchaguzi," alisema Mwakagenda.
Aidha,
Mwakagenda alisema uvamizi huo uliathiri na kuwafanya wakashindwa
kukusanya taarifa za mwisho za uangalizi wa matokeo na ukusanyaji wa
maoni ya wananchi.
"Uangalizi
kwa kutumia tehama haujaanza mwaka huu kwani, tangu mwaka 2010 kulikuwa
na utaratibu huu, mambo yaliyofanyika hivi sasa tunashindwa kuelewa
tatizo ni nini," alisema. |
No comments:
Post a Comment