PICHA NA BIMA YA AFYA YA KIKOA

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona akizungumza wakati akifungua kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo wa Mirerani, (kushoto) ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) wa mkoa huo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa Tarafa ya Moipo Joseph Mtataiko.

Vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wa Vicoba, Saccos na wasindikaji ngozi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa (Kikoa).

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) wa Mkoa wa Manyara, Isaya Shekifu akizungumza katika kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro kushoto ni mkuu wa wilaya hiyo Mahmoud Kambona na kulia ni mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii (CHF) mkoani humo Reginald Kileo.

Post a Comment

أحدث أقدم