Pages

November 7, 2015

PAPA WEMBA NDANI YA BONGOLAND

Mwanamuziki Papa Wemba (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake waandaaji wa Tamasha la Karibu Music Festival 2015 mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie akimtambulisha kwa wenyeji wao.
Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.
Mapozi ya wanenguaji wa Papa Wemba katika picha mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kutumbuiza katika tamasha la Karibu Music Festival 2015.
Mwanamuziki Papa Wemba akiwa katika picha ya pamoja na wasanii alioambatana nao waliomo katika bandi yake mara baada ya kutua Tanzania tayari kufanya mashambulizi katika Tamasha la Karibu Music Festival 2015 linalofanyika Bagamoyo.
Msafara wa mwanamuziki Papa Wemba ukipokewa na wenyeji wao mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA).
Mwanamuziki Papa Wemba (kushoto) akiwa na Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie (kulia) mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...