Pages

November 8, 2015

Maalim Seif: Hakuna namna ya kupindua maamuzi ya wananchi kupitia kura


 Katika Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi wa Wilaya na Majimbo wa Chama hicho katika Ukumbi wa Majid, Kiembesamaki Zanzibar.
 Viongozi wa Wilaya na Majimbo wa CUF, wakimsikiliza katiba mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika Ukumbi wa Majid, Kiembesamaki Zanzibar.
Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi CUF Taifa Bw. Twaha Taslima, akisoma maazimio ya baraza kuu kwa waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho Vuga mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR).
 

Na: Hassan Hamad, OMKR

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka wafuasi na wapenzi wa Chama hicho kutembea kifua mbele kutokana na ushindi mkubwa walioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita.

Amesema ushindi huo umeleta matumaini mapya kwa wazanzibari ambao wameitumia vyema haki yao ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaoataka.

Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu ngazi za Wilaya na Majimbo katika ukumbi wa Majid Kiembesamaki Zanzibar, Maalim Seif amesema hakuna namna yoyote ya kupindua maamuzi ya wananchi waliyoyafanya kupitia masanduku ya kura.

Amesema wanachokifanya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar hivi sasa ni kuchelewesha kukamilisha uhakiki wa kura kwa majimbo 14 yaliyobakia na kumtangaza mshindi wa Urais, na hivyo kuishauri tume hiyo kukamilisha zoezi hilo ili serikali mpya ianze kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi.

“Mimi sina wasi wasi, ninajihesabu kama Rais ninayesubiri kuitwa na kuapishwa, na sasa nimo katika matayarisho ya kuunda serikali ili nikiapishwa tu nisipoteze tena muda wa kufikiria kuunda serikali”, alisema Maalim Seif katika kikao hicho cha kwanza cha kuzungumza na wajumbe hao tangu uchaguzi mkuu wa Zanzibar ulipomalizika.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...