Pages

November 9, 2015

ARDHI YAPASUKA HUKO MISSISSIPPI NCHINI MAREKANI NA KUMEZA MAGARI 12


Vipimo vitafanywa kubaini kwanini aridhi imepasuka na kumeza magari 12 huko Mississippi nchini Marekani katika eneo la maegesho ya magari kwenye hoteli moja.
Shimo hilo la kupasuka ardhi lenye urefu wa mita 120 na upana wa mita 11 lilifunguka jumamosi huko Meridian, karibu na jimbo la Alabama.
Eneo hilo lilipata mvua kubwa kwa wiki mbili zilizopita, gazeti la Meridian Star limeandika. Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Magari yakiwa yametumbukia aridhini baada ya ardhi kupasuka
Gari likiwa limenusurika kidogo kutumbukia baada ya ardhi kupasuka

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...