Mgombea
Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) akiungwa mkono na vyama vinne vinavyounda vuguvugu la Umoja wa
Katiba ya Wananchi, UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akimsalimia Bi. Lemmy
Mahogija (albino) na Mtoto wake Zawadi Elias, wakati alipowasili kwenye
Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Masumbwe, Jimbo la Mbogwe, Mkoani Geita Oktoba 14, 2015. Mheshimiwa
Lowassa na timu yake ya kampeni, wameendelea kuimarisha kampeni zao
katika kipindi hiki cha lala salama, ambapo tayari amekwisha zunguka
karibi mikoa yote nchini, na anatarajiwa sasa kutua mkoani Pwani na
kampeni zake zitakamilika mkoani Mbeya, kabla ya upigaji kura ambapo
Watanzania wataamua hapo Oktoba 25, 2015 sawa na siku 11 tu zimesalia.
(Picha na Othman Michuzi).
Mh. Lowassa akihutubia maelfu ya wananchi kwenye viwanja hivyo
Mh. Edward Lowassa akifurahi na Mtoto Anne Masanja
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akihutubia mkutano huo wa kampeni





Post a Comment