Pages

September 15, 2015

VIJANA WAMETAKIWA KUTUMIA MAZINGIRA YANAYOWAZUNGUKA KUJIPATIA KIPATO

  Afisa vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw.Godfrey Massawe akizungumza na wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kabla ya kufunga mafunzo ya wawezeshaji hao leo Jijini Mwanza. 
 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru akizungumza na Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha (hawapo pichani) kabla ya kufunga Mafunzo ya siku nane ya Uwezeshaji kwa wawezeshaji hao leo Jijini Mwanza. Kushoto ni Afisa Vijana Bw. Godfrey Massawe na kulia ni Mwezeshaji Kitaifa Bibi. Octavina Kiwone
 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru  akitoa cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Uwezeshaji wa Stadi za Maisha  kwa Bw. Edwin Gacho (kushoto) wakati wa kufunga Mafunzo hayo leo Jijini Mwanza
 Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Diana Kasonga (kushoto) akifuatilia Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka Mkoa wa Kagera wakiandaa Mpango kazi watakaotumia wakati wa kufikisha ujuzi walioupata kwa waelimisha rika wa  Mkoa wa Kagera.
 Mwezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha Bi. Virginia Chacha (kulia) akifanya mazoezi ya uwezeshaji kwa wawezeshaji wenzake kama njia mojawapo ya kupima uwezo wa wawezeshaji hao kabla ya kufunga Mafunzo ya Uwezeshaji leo Jijini Mwanza
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru (wapili kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha baada ya kufunga mafunzo ya uwezeshaji leo Jijini Mwanza. Wapili kulia ni Mtaalam wa Stadi za Maisha Bw. Benny Lugoe na wakwanza kulia ni Afisa Vijana Bw. Godfrey Massawe.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mwanza


Na: Genofeva Matemu - Maelezo, Mwanza
Vijana wametakiwa kutumia vizuri mazingira wanayowazunguka kuibua mbinu mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kuondoka na taifa tegemezi kwa kusubiri kuajiriwa mara baada ya  kuhitimu masomo yao.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru alipokua akifunga mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha leo Jijini Mwanza.
Bibi. Ndunguru amesema kuwa vijana waliopata mafunzo ya uwezeshaji wa stadi za maisha ni mabalozi ambao kama watatumia vizuri uwezo walioupata katika mafunzo hayo watabadili fikra za vijana wengi nchini hivyo kuweza kujenga taifa lenye afya nzuri, weledi na pamoja na ujuzi.
Kwa upande wake Mtaalamu wa masuala ya Stadi za Maisha Bw. Benny Lugoe amesema kuwa  washiriki wa Mafunzo ya Stadi za Maisha wana ari na motisha ya kujifunza na kama wataendelea kuwa na ari hiyo watakua wabunifu na wawezeshaji wazuri kwa vijana ndani ya jamii.
Aidha  Bw. Lugoe amewataka wahitimu wa kitaifa wa Stadi za Maisha kutimiza wajibu wao kwa kuwaandaa waelimisha rika katika mikoa yao ili kuweza kutimiza malengo yaliyokusudiwa na kuweze kubadili fikra za vijana katika jamii.
Naye Mwezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka Mkoa wa Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga amesema kuwa ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ni tatizo kubwa kwa Mkoa wa Shinyanga hivyo ugeni wa mafunzo ya stadi za maisha katika Mkoa huo utawavutia vijana wengi jambo ambalo litapelekea kutimiza lengo la serikali kufikisha mafunzo hayo kwa vijana wa rika mbalimbali.
Bw. Manjerenga ameiomba serikali kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wawezeshaji wa kitaifa wa Stadi za Maisha haswa pale panapokua na mabadiliko katika mwongozo wa Stadi za maisha ili kuweza kubadilisha fikra za vijana wote nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...