|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Mke
wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete akizungumza na umati wa wanaCCM na
wapenzi wa chama hicho uliokuwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja
nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea
mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Katibu,
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na wanaCCM na
wananchi kwenye mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia
Suluhu jana Mkoani Lindi. |
|
Bi.
Samia Suluhu (kulia) akimtambulisha mgombea mmoja wa wagombea udiwani
katika Jimbo la Mchinga, kuzungumza na wapiga kura wa eneo hilo. |
|
Samia Suluhu akimpokea mmoja wa wanachama mpya aliyejiunga na CCM katika Jimbo la Mchinga. |
|
Bi. Samia Suluhu akimpokea mmoja wa wanachama mpya aliyejiunga na CCM katika Jimbo la Mchinga. |
|
Mmoja wa wanachama wapya wa CCM aliyejiunga na CCM mara baada ya mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza katika Jimbo la Mchinga. |
KAMPENI
za mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Bi. Samia Suluhu zinazoendelea mkoani Lindi zimekuwa tishio kwa vyama
vya upinzani baada ya mkutano uliofanyika jana eneo la Mnazi Mmoja nje
kidogo ya mji wa Lindi Mjini kuzoa wanachama 61 waliotoka upinzania na
kujiunga na CCM.
Mkutano
huo wa kampeni uliohudhuriwa pia na Mke wa Rais Mama Salima Kikwete
umeacha maumivu kwa vyama vya upinzani vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi
baada ya kujikuta wanachama 61 wakivikimbia vyama vyao na kujikuta
wakijiunga na Chama Cha Mapinduzi na kukabidhiwa kadi mpya za CCM kila
mmoja.
Miongoni
mwa wanachama ambao walipokelewa leo ni pamoja na Katibu wa Chadema
Wilaya ya Lindi Mjini, Abdullah Madebe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mtaa
wa Nananji Lindi, Bakari Kalulu na wanachama wengine kutoka vyama vya
CUF na Chadema. Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi, Bi. Samia Suluhu
Katibu wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini alisema awali alipokuwa upinzani
alikuwa amepotea na amegunduwa kuwa alikuwa anapoteza muda hivyo kuomba
wananchi wamsamehe na ameamua kurudi kundini na kuendelea kulkijenga
taifa.
Akizungumza
baada ya kuwapokea wanachama hao, mgombea mwenza Suluhu alisema
Serikali ya awamu ya tano imeandaa mambo mengi mazuri kwa mikoa ya Lindi
na Mtwara na jambo la kwanza kulifanya baada ya kuunda serikali ni
kuubadili mji wa Mtwara na Lindi kuwa miji ya viwanda, hali ambalo
itakuza uchumi kwa kiasi kikubwa hivyo kunufaisa wananchi.
Alisema
kwa kuanzia Serikali inajenga viwanda vinane mkoani Mtwara na vingine
vitajengwa mkoani Lindi viwanda ambavyo vitategemea gesi katika
uzalishaji wake bidhaa ambayo tayari inapatikana kwa wingi katika maeneo
hayo. Alisema ujenzi wa viwanda utaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na
kuongeza nafasi za ajira jambo ambalo litawanufaisha wakazi wa eneo hilo
na wawekezaji.
"...Tunataka
kuitenga Lindi kuwa mji wa viwanda vitakavyoitumia gesi kwa uendeshaji,
lengo ni kuwa na viwanda vitakavyozalisha nafasi za ajira takribani
asailimia 40...," alisema Bi. Suluhu. Awali akihutubiwa katika mkutano
wa kampeni ulofanyika Kata ya Mingumbi Kilwa Kusini, alisema Serikali
inatambua hali ya kuyumba kwa soko la korosho na ufuta ili kukabiliana
na hali hiyo imejipanga kujenga viwanda vya kubangua na kufunga korosho
pamoja na kukamua mafuta kwa lengo la kumuongezea thamani mkulima katika
zao analozalisha.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara wa Mnazi Mmoja Katibu, Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nape Nnauye aliwatoa hofu akinamama na wapiga kura wengine juu ya
vitisho vya kuwepo na vurugu kipindi cha uchaguzi kwa lengo la kuwatisha
wapiga kura, hivyo kuwataka wananchi wasiogope kwani Serikali na CCM
kupitia vijana wake imejipanga kupambana na wafanya fujo hao.
Alisema
kitendo cha kutoa vitisho kwa wapiga kura ni kuibaka demokrasia hivyo
CCM na vijana wake hawatakuwa tayari kuona demokrasia inabakwa nchini na
wapuuzi wachahe. "...Vijana wa CCM naomba mkikamata kibaka wa
demokrasia shughulikeni naye kidogo kabla ya kumpeleka polisi...CCM
itashinda kwa kishindo," alisema Nape Nnauye.
Aidha
msemaji huyo wa Chama Cha Mapinduzi alisema mgombea urais wa Chadema,
Edward Lowassa pamoja na mpambe wake anayemuunga mkono Fredrick Sumaye
hawawezi kuiponda Serikali ya CCM kwa kuwa wao wamekuwemo na kushika
nafasi za juu za utendaji ndani ya serikali na kama walishindwa kuleta
mabadiliko hawawezi kufanya hivyo leo.
Aliongeza
kuwa kitendo cha kuendelea kuiponda ni sawa na kujidhalilisha wao
wenyewe kwa wananchi hivyo kuwataka wasiwarubuni Watanzania kwamba
wanamabadiliko ya msingi zaidi ya maslahi yao binafsi, ambayo ndiyo
yanayowasukuma kukimbilia walipo.
Mgombea
mwenza wa urais CCM, Bi. Suluhu bado anaendelea na ziara ya kuinadi
ilani ya Chama Cha Mapinduzi Mkoani Lindi na baada ya kumaliza majimbo
ya mkoa huo ataendelea katika Mkoa wa Mtwara, kuwashawishi wananchi
kuichangua CCM ili iweze kupata ridhaa ya kuunda Serikali ya awamu ya
tano.
|
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu kwenye Jimbo la |
|
Kutoka
kushoto ni mgombea mwenza wa CCM nafasi ya uraisa, Bi. Samia Suluhu na
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Maiza na mgombea wa Jimbo la Mchinga
Said Mtanda wakiwa kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo la Mchinga
jana. |
|
Mgombea
Jimbo la Mchinga Said Mtanda akizungumza na wannaCCM na wananchi jana
jimboni kwake ambapo mgombea mwenza alihutubia wananchi. |
|
Sehemu ya wanaCCM na wananchi jana jimboni kwake ambapo mgombea mwenza alihutubia wananchi. |
|
Mbunge
wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Anjela
Kiziga akizungumza katika mkutano wa kampeni za CCM. |
|
Aliyekuwa
Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Chadema Taifa, Greison Nyakarungu ambaye
kwa sasa amejiunga na CCM akizungumza katika moja ya mikutano ya kampeni
ya CCM. |
|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza akizungumza na wanaCCM na wananchi
kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu. |
|
Mke
wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi,
Mzee Ally Mtopa pamoja na mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi.
Samia Suluhu wakijadiliana jambo kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea
mwenza wa CCM viwanja vya Mnazi Mmoja. |
|
Sehemu
ya umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika
uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa
kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Katibu
wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini, Abdullah Madebe akikabidhi kadi ya
chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). |
|
Aliyekuwa
Katibu wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini, Abdullah Madebe (kulia)
akipongezwa na Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu
mara baada ya kujiunga na CCM, Katikati ni Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete. |
|
Mmoja wa wananchi waliojiunga na CCM katika mkutano huo akizungumza baada ya kujiunga na chama hicho tawala. |
|
Mama Salma Kikwete pamoja na Bi. Samia Suluhu wakipokea kadi za wanachama waliojiunga na CCM jana Mkoani Lindi. |
|
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Mzee Ally Mtopa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM viwanja vya Mnazi Mmoja. |
|
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM pamoja na wananchi viwanja vya Mnazi Mmoja. |
|
Kada
wa CCM na mbunge wa zamani wa Mchinga, Mudhir Mudhir akizungumza na
wanaCCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Mchinga katika mkutano wa
kampeni. |
*Imeandaliwa/www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment