Waziri Membe akiendelea kuzungumza |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Tunsume Mwangolombe (katikati) naye akifuatilia ufunguzi wa Semina hiyo. |
Sehemu ya wadau wakifuatilia ufunguzi wa Semina hiyo |
Semina ikiendelea |
Waziri Membe (katikati) na Waziri Maeland kwa pamoja na wajumbe waliofuatana nao wakiwa kwenye mazungumzo mara baada ya kumaliza ufunguzi wa semina. |
Waziri Membe (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya faida ya semina hiyo ya wafanyabiashara wa Tanzania na Norway |
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea |
TANZANIA NA NORWAY KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI
Waziri
wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
ameisifu Serikali ya Norway kwa kuwa mshirika wa karibu wa maendeleo wa
Tanzania hususan katika sekta za biashara na uwekezaji.
Waziri
Membe alitoa kauli hiyo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara,
Mhe. Abdallah Kigoda wakati akifungua rasmi semina kuhusu kuimarisha
ushirikiano wa Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Norway
iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam leo.
Katika
ufunguzi huo ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Biashara na Viwanda wa
Norway, Mhe. Monica Maeland ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi,
Mhe. Membe alisema kuwa Tanzania na Norway zimekuwa na ushirikiano wa
kidiplomasia kwa miaka mingi lakini sasa nchi hizi zimeamua kushirikiana
zaidi katika masuala ya uwekezaji na biashara ili kukuza uchumi kwa
maendeleo ya nchi zote mbili.
Aliongeza
kuwa, kwa miaka mingi Tanzania imefaidika na ushirikiano na Norway
katika sekta mbalimbali ambapo nchi hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa
katika kuisaidia Tanzania kupambana na umaskini na kukuza uchumi. Hata
hivyo alisema umefika wakati sasa nchi hizi mbili zinufaike kupitia
biashara na uwekezaji ambapo nchi zote zina fursa nyingi katika maeneo
hayo ikiwemo gesi na mafuta, kilimo na madini.
Mhe.
Membe alisema kuwa kufanyika kwa semina hii itakayowakutanisha
wafanyabiashara na wawekezaji itaongeza thamani katika uhusiano wa
kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili ambapo Tanzania ina mengi ya
kujifunza kutoka Norway ambayo ni miongoni mwa nchi zinazosafirisha
zaidi gesi asilia na mafuta duniani. Hivyo aliwaasa Watanznaia kutumia
semina hiyo kujifunza ili kuimarisha sekta ya nishati ya hapa nchini.
“Semina
hii ni fursa kwa Kampuni za Tanzania na Norway kujifunza na kubadilisha
uzoefu na mawazo ya namna bora ya kuboresha sekta za biashara na
uwekezaji kwa manufaa ya nchi zote mbili” alisema Waziri Membe.
Akizungumzia
biashara inayofanyika kati ya Tanzania na Norway, Mhe. Membe alisema
kuwa Tanzania inatakiwa kuongeza biashara yake nje ya nchi ili
kuimarisha uchumi wake. Alieleza kuwa kwa sasa biashara kati ya Tanzania
na Norway imeongezeka kutoka shilingi bilioni 1.6 mwaka 2010 hadi
kufikia shilingi bilioni 6.9 mwaka 2014 kwa bidhaa zilizozwa Norway
kutokea Tanzania ikiwemo kahawa, chai, viungo, maua, mbogamboga, mbao na
madini.
Kwa
upande wa bidhaa kutoka Norway, Tanzania imenunua kwa ongezeko la
kutoka bilioni 22.3 mwaka 2010 hadi kufikia shilingi bilioni 73 mwaka
2014. Bidhaa hizo ni pamoja na dawa za binadamu na bidhaa za viwandani.
Kwa
upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara wa Norway, Mhe. Monica
aliipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika maendeleo na ukuaji
wa uchumi ambao umefikia asilimia 7. Alieleza kuwa Tanzania itafikia
azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa vile
inayo dhamira ya dhati na imejipanga kupitia uvumbuzi wa gesi na mafuta,
nguvukazi ya vijana na mageuzi yaliyopo katika sekta ya uchumi.
Alieleza
kuwa Norway ipo tayari kuendelea kuisadia Tanzania katika sekta ya gesi
na mafuta kwa vile nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika eneo hilo
hususan katika masuala ya teknolojia. Aidha, aliongeza kuwa Tanzania ni
mshirika wa kweli wa Norway katika maendeleo hivyo nchi yake
itashirikiana kikamilifu na Tanzania.
“Kuna
msemo maarufu unasema kama unataka kwenda mbio nenda peke yako, lakini
kama utanaka kufika mbali nenda pamoja na mwenzako. Hivyo Norway inataka
kwenda pamoja na Tanzania ili kuziwezesha nchi hizi kufika mbali
kimaendeleo” alisisitiza Mhe. Monica.
Awali
akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Balozi wa Norway hapa
nchini Mhe. Hanne-Marie Kaarstad alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa
nchi hizi mbili kukuza biashara kwa kuishirikisha sekta binafsi
kikamilifu kwani ni nyenzo muhimu kwa maendeleo endelevu.
Semina
hiyo ambayo imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Norway,
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Shirikisho la Wenye Viwanda
Tanzania (CTI) ilihudhuriwa na Makampuni 34 kutoka Norway na Tanzania na
pia wadau mbalimbali wa biashara na uwekezaji.
No comments:
Post a Comment