Hii taarifa imegusa Vichwa vya Habari
vya Vyombo vingi vya habari Duniani, inahusu ajali ambayo imetokea
wakati watu wakiwa ndani ya Msikiti Mtakatifu wa Mecca, Saudi Arabia
ambako waumini wengi wa Dini ya Kiislamu huwa wanakwenda kwa ajili ya
Hijjah.
Ajali hiyo inahusisha winch kubwa ambalo
lilikuwa likitumiwa kwenye ujenzi eneo la jirani na Msikiti huo
kuangukia Msikiti huo, ambapo kwa wakati huo kulikuwa na watu zaidi ya
800 wakiendelea na sala ndani ya Msikiti.
Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu
usalama wa watu wanaoenda kwenye Msikiti huo kutokana na maeneo
yanayozunguka Msikiti kuna majengo mengi yanayoendelea kujengwa na
kukarabatiwa pamoja na Msikiti wenyewe kufanyiwa ukarabati wa upanuzi
ili kuweza kungiza watu wengi zaidi.
Mpaka sasahivi Ripoti zinaonesha zaidi
ya watu 100 wamefariki, wengine zaidi ya 200 wamepata majeraha
na Mamlaka za Mji huo wanasema sababu hasa za winch hilo kuanguka
inatokana na upepo mkali pamoja na mvua kubwa.



إرسال تعليق