Pages

September 23, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE ATOA ZAWADI YA IDD KWA MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA

Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda(wa pili kulia)kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi za Idd el Hajj Meneja wa Mahabusu ya Watoto mkoa wa Arusha,Mussa Mapua leo kwaajili ya kusherekea siku kuu hiyo kesho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete ametoa zawadi mbalimbali katika Mahabusu ya watoto walikinzana na sheria iliyopo jijini Arusha.

Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Kikwete,Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda amesema pamoja na kuwa watoto hao wanakabiliwa na mashtaka ya kujibu lakini mheshimiwa Rais anatambua haki zao za kushiriki na jamii kufurahia siku kuu hiyo ya kidini.

"Kama mnavyofahamu Rais Kikwete amekua na utamaduni wa kuwakumbuka katika siku kama hizi ili nanyi mfurahie siku kuu hii,"alisema Mapunda

Akipokea zawadi hizo Meneja wa Mahabusu hiyo,Mussa Mapua amesema imekua ni faraja kwa kiongozi wa nchi kuwakumbuka na kuomba taasisi nyingine na watu binafsi kuiga mfano huo na kumtakia Rais Kikwete mapumziko mema anapojiandaa kumaliza muhula wa pili wa uongozi wake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...